Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Aref Nahdi,
kulia akikabidhiwa Tuzo na Balozi wa
Pakistani, Amiri Muhammad Khan wapili kushoto, wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya ilala Charles
Kuyeko, na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Alhuda Center of Islamic
Banking and Economics, ya nchini Dubai Muhammad Zuberi ambao ndiyo waliotowa
Tuzo hiyo.
....................................
Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation
Aref Nahdi amekabidhiwa Tuzo na Shirika la Kimataifa linalotoa mafunzo kwa Benki za
kiislamu na kusimamia Uchumi wa
kiislamu la Alhuda Center
of Islamic Banking and Economics, (CIBE) ambalo Makao yake makuu nchini Dubay.
Tukio hilo limefanyika katika Mkutano wa kujadili Uchumi wa Kiislamu
na Changamoto zake kwa nchi za Afrika ambao umeandaliwa na CIBE, mkutano
uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regence jijini Dar es Salaam
Akizungumza
mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwenyekiti wa The Islamic Foundation Aref Mubaarak Nahdi,
amesema zawadi hiyo imetolewa kutokana na kutambua mchango wa The Islamic
Foundation katika jamii na kusema kuwa hiyo inatoa fursa kwa Taasisi ya The Islamic Foundation kuongeza
juhudi.
Alisema The Islamic Foundation
inatekeleza wajibu wake kwa kumuogopa Mwenyezimungu na wala sio kwa kuwaangalia watu na kwamba juhudi zinazofanywa na The Islamic Foundation ni kielelezo tosha kwenye uso
dunia kwamba The Islamic Foundation
inatekeleza wajibu wake.
Aliongeza kwa kusema kwa kujiangalia mwenyewe huwezi kujua ukubwa wa mambo
unayofanya lakini sifa na pongezi zinazotolewa na watu ndio
zinazopelekea kutambua kuwa TIF
inafanya mambo makubwa hapa
nchini.
Aidha,
aliwataka watendaji wote wa The
Islamic Foundation kwenye kila kitengo
kuongeza juhudi ya utendaji
kazi ili
kufanikisha malengo ya kuutumikia
uislamu na kuongeza kuwa malipo yake
hayawezi kupimwa kwa macho ya kawaida na
kwamba faida ya kuitumikia TIF kwa maslahi ya uslamu ni yamilele.
Mwenyekitihuyo wa The Islamic Foundation amepokea Tuzo
hiyo kutokana na kazi
zinazofanywa na Taasisi anayoingoza kutekeleza majukumu
yake kwa juhudi kubwa ya kueneza
Elimu kwa jamii ya Kiislamu na wananchi kwa ujumla.
Akielezea wakati wa kukabidhiTuzo hiyo mzungumzaji kutoka
shirika lakimataifa la Alhuda alisema Tuzo hiyo inakwenda kwa Aref
Nahdi kutokana na mchango wake
mkubwa katika kuupeleka
mbele uislamu ambao mpakasasa
inamiliki Hospitali, Shule za Msingi
na Sekondari, Gazeti, Kituo cha Redio na Tevisheni.
Aliongeza kuwa katika idara zake za Elimu TIF pamoja na vyombo
vyake vya Habari imekuwa mstari wa mbele katika kutoa Elimu inayopelekea watu kujua
ubaya wa riba na kupelekea watu wengi
kuongeza ufahamu kuhusu madhara ya Riba
na kufahamu njia sahihi za kukuza Uchum
kwa mujibu wa uislamu.
Mkutano huo
wa siku mbili wa kujadili Uchumi
wa Kiislamu Afrika umehuduriwa na nchi
kumi zaidi ya kumi ambapo kwa
pamoja wamekubaliana kuongeza Elimu juu ya matumizi ya
Benki za kiislamu, Uharamu wa Riba
na kuzitaka Serikali za nchi za Afrika kutunga Sheria
zitakazosimamia uendeshaji wa Benki za
Kiislamu.
Miongoni
mwa Taasisi zilizopata Tuzo ni
Amana Bank, Ibni Jazari, ZIC Takaful, IFM, NBC ISLAMIC WINDOW, ICCIU Uganda, Gulf African Bank,
Nairobi, FSDT, Dar es Salaam.
Mezani ni tuzo aliyopewa Mwenyekiti wa The
Islamic Foundation (TIF) Aref Nahdi.
Mkurugenzi wa Amana Bank, Dkt. Muhsin Masoud kulia akikabidhiwa Tuzo na Balozi wa
Pakistani, Amiri Muhammad Khan wapili kushoto, wa pili kulia ni Meya wa Manispaa ya ilala Charles
Kuyeko, na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Alhuda Center of Islamic
Banking and Economics, ya nchini Dubai Muhammad Zuberi ambao ndiyo waliotowa
Tuzo hiyo.
Mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Aref Nahd
kulia, akikabidhi cheti kwa Mwenyekiti wa ZIC Takaful, Dkt. Muhammad Hafidhi
Khalifa.
No comments:
Post a Comment