Rais
Mstaafu wa awamu ya nne, Jakakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo
wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa kwa mkewe mama
Salma.
.......................
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wamelipuka kwa shangwe kufuatia Spika wa Bunge hilo kumtambulisha Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara alipowasili Bungeni
hapo kwaajiliya kushuhudia kuapishwa kwa mkewemama Salma Kikwete.
Baadhi ya wabunge wamesikika wakisema kuwa
wamemmisi Rais Mstaafu huku wengine wakisema rudi baba na wengine wakitaka
aruhusiwe kuingia eneo la wabunge iliawsalimie kwa kuhutubia.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jobu Ndugai alisema katika kipindi chote alichokaa Bungenihaijawahi kutokea
mgenikupokelewa kwashangwe kama JK.
Picha ya video iliyokuwa ikionyesha namna wabunge
wakimshangilia Rais huyo Mstaafu wa awamuya nne ilionekana wabunge wote kuwa na furaha na
mapenzi makubwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete hata wale wa upinzani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa Rais wa awamu
ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo alitawala vipindi viwili kwa
muda miaka10 na kumaliza utawala wake kwa mujibu washeria mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment