Serikali imeipongeza Serengeti Boys kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mechi
ya kirafiki dhidi ya Gabon.
Serengeti Boys wameifunga Gabon katika mechi iliyopigwa nchini Morocco
ambako timu hiyo imeweka kambi kujiandaa na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika
litakalofanyika nchini Gabon.
Msemaji wa Serikali Dk, Hassan Abbas amesema serikali inaipongeza timu
hiyo ya vijana chini ya miaka 17 kwa ushindi huo.
Serikali inawasisitiza vijana hao kuendelea kupambana wakiwa wamelenga
kufanya vizuri na Watanzania na serikali iko nyuma yao.
No comments:
Post a Comment