Spika
wa Bunge Mh. Job Ndugai , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mhe. Ummy na Mkuu wa wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius Ndejembi wakikata
utepe kuashiria uzinduzi wa mpango huo .
Spika
wa Bunge Mh. Job Ndugai akipokea vitanda hivyo kutoka kwa Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy , kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius Ndejembi.
Spika
wa Bunge Mh. Job Ndugai , Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Mhe. Ummy , kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kongwa Bw.Deogratius
Ndejembi.wakikagua vitanda hivyo mara baada ya makabidhiano.
..................
Serikali ya awamu ya tano nchini imezindua rasmi usambazaji wa vifaa vya
hospitali kwa halmashauri zote nchini katika kutekeleza mkakati wa
kuboresha huduma za afya nchini kwa kuhakikisha wananchoi wanapata huduma kwa
kiwango stahiki.
Akizindua usambazaji huo leo wilayani hapa,Waziri wa Afya,maendeleo
ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu alisema serikali imetekeleza ahadi
iliyotoa kwa wananchi ambapo serikali inawekeza katika afya ya wananchi
hivyo kuweza kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Akizungumza kwenye hadhara ya wanachi wa Wilaya ya Kongwa,Waziri Ummy
alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo ya
upatikanaji wa dawa ambapo bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi bilioni
31 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 251 mwaka 2016/17.
“Hatua hii imeleta mapinduzi makubwa katika upatikanaji wa dawa,vifaa na
vifaa tiba kwenye vituo vya Umma vya kutolea huduma za afya,hivyo wanaomba
wananchi kuhakikisha mnafika kwnye vituo vya kutolea huduma za afya ili kupata
matibabu sahihi”.
Aidha, Waziri Ummy alisema kufuatia ahadi ya Mhe. Rais ya kununua na
kusambaza vitanda kwenye vituo vya Umma ,Wizara yake kwa bajeti ya mwaka
2016/17 ilitenga kiasi cha shilingi biliuoni 4 za kuwezesha kununua pamoja na
kusambaza vifaa hivyo kwa halmashauri 184 nchini
Alivitaja vifaa vilivyonunuliwa na kuvikabidhi kwa Mhe. Job Ndungai (Mb),
Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungazo wa Tanzania
Mhe. John Ndugai ni pamoja na vitanda vya hospitali
(20),vitanda vya kujifungulia wajawazito (5), magodoro (25) na mashuka (50).
Vifaa vya Hospitali vitakavyopasambazwa kwenye Halimashauri zote 184
nchini ni pamoja na vitanda vya hHospitalini 3,680; vitanda vya kujifungulia
akinamama wajawazito 920; magodoro 4,600; na mashuka 9,200. Thamani ya vifaa
hivi ni shilingi bilioni 2,933, 125,600. Zoezi la kugawa vifaa hivi
linatarajiwa kukamilika kabla ya Juni 30, 2107.
Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Ndugai ameishukuru Serikali kwa msaada wa
vifaa vilivyotolewa kwa Hospitali na vituo vya Afya katika mkoa wa Dodoma
ikiwemo Halmashauri Kongwa. Vifaa hivyo vitaboresha afya ya wananchi wa jimbo
la Kongwa na maeneo mengine nchini na hivyo kusaidia kuwawezesha wananchi
kukutumia mudao wao mwingi katika shughuli za kiuchumi.
No comments:
Post a Comment