Uongozi wa klabu ya Mbao FC ya
Ilemela jijini Mwanza umemsimamisha mlinda mlango wa timu hiyo Erick Ngwengwe
kwa muda usiojulikana kwa tuhuma za upangaji wa matokeo kwa madai kuwa
amechukuwa rushwa kwa klabu ya Simba au kuwa na mapenzi binafsi na Simba.
Afisa Habari wa Mbao FC,Christian
Malinzi ameuambia mtandao huu kuwa katika kikao kilichoketi siku ya jana
uongozi umeamua kumsimamisha kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi zaidi
juu ya kile kinachoenekana amehusika katika upangaji wa matokeo.
Malinzi alisema kwamba uongozi
ulijalibu kutafuta dodosa za tuhuma hizo,umebaini kuwepo kwa viashiria vya
upangaji wa matokeo ambavyo vimesababishwa na yeye kwa kuweza kuruhusu magoli
ya kizembe.
Alisema kwamba kwa sasa hawawezi
kumtuhumu moja kwa moja kuwa ndie aliyehusika na swala hilo ndio maana uongozi
umeamua kumuondoa kambini ili kupisha uchunguzi wa kina juu ya yake.
Hata hivyo alisema kwamba ingawa
hakuna taarifa ya kuhusika katika swala la kuchukua fedha lakini huenda
kukawepo na mapenzi binfsi kwa mchezaji mwenyewe kuipenda timu Pinzani kwani
wachezaji wengi wa Tanzania wamegawanyika katika vilabu vya Simba na Yanga.
No comments:
Post a Comment