Tume ya Taifa
ya Uchaguzi inapenda kuutarifu Umma kuwa; kwa mujibu wa Kifungu cha 37 (3) cha
Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa;
kufuatia Mbunge wa Viti Maalum, SOPHIA MNYAMBI SIMBA kufukuzwa
uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.
uanachama wa Chama cha Mapinduzi tarehe 11 Machi, 2017 kiti cha Mbunge huyo wa Viti Maalum Wanawake kwa tiketi ya CCM kiko wazi.
Kwa mujibu
wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya Ubunge ni lazima awe mwanachama
aliyependekezwa na Chama chake husika
cha Siasa.
Kwa kuwa Ndg. SOPHIA MNYAMBI SIMBA amefukuzwa uanachama wa Chama
kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa Mbunge huyo amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea Ubunge.
Kutokana
na kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge wa
Viti Maalum, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu
cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Jaji
(R) Semistocles Simon Kaijage
(R) Semistocles Simon Kaijage
Mwenyekiti
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI
YA TAIFA YA UCHAGUZI
No comments:
Post a Comment