Mkurugenzi wa Alhuda Center Of Islamic Banking
and Economics, Muhammad Zuberi akiwasilisha mada katika mkutano huo.
...........................
Uchumi wa Kiislamu Afrika unakabiliwa na
changamoto za kukosekana kwa sheria maalum zinazosimamia Benki za Kiislamu
pamoja na uelewa mdogo miongoni mwa
jamii.
Wakizungumza
wakati wa kuwasilisha mada washiriki mbalimbali wa mkutano wa kujadili
Uchumi wa Kiislamu Afrika, uliofanyika
jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, wamesema Benki za kiislamu Afrika hazina sheria
maalum kutoka serikalini za
kuwasimamia kutekeleza majukumu yao
kikamilifu.
Wamesema mfumo
unaotumika hivisasa katika
kuendesha Benki za
Kiislamu katika nchi za Afrikani
uleunaotumikakuendesha Benki za kawaida
zinazotumiaRiba hali inayopelekea kukwama katika baadhiya mambo
kwenye utekelezaji.
Wameongeza kuwa miamala mbalimbali ya kifedha
kwa mujibu wauislamu haipati
msaada wa sheria za serikali ili kuwa na
nguvu katika usimamizi wa miamala hiyo kwa mujibu wa sheria
za nchi.
Walisema
utekelezaji wa sheria za kiislamu
hauhitaji msaada wa
sheria zingine lakini katika miamala ya kifedha ambayo mara nyingi inahitaji dhamana na
uwezeshwaji kutoka serikalini ni
wazi kuwa bilaya kuwa na shria maalu inayosimiamia miamala ya
kiefdha kwa mujibu wa uislamu bado kutakuwa na changamoto
nyingi katika kufikia malengo.
MCHANGO WA BENKI
ZA KIISLAMU KATIKA KUKUZAUCHUMI.
Wakizungumzia mchango wa Benki za kiislamu katika
kukuzaUchumi, washiriki hao walisema
Benki za kiislamu zina mchango mkubwa
sio tu katika kukuza uchumi
wa kiislamu lakini
pia hata katika kuchangia miradi ya maendeleo ya
nchi ambapo nchi mbalimbali zimefaidika
na mfumo wa Benki za kiislamu.
Walitolea mifano ya nchi ambazo zimefaidika
na mfumo
wa Benki za kiislamu katika
kuchangia maendeleo ya serikali ni pamoja
na Afrika ya kusini, Togo,
Nigeria ambapo wametumia njia ya Benki za
kiislamu kuweza kutekeleza miradi
ya maendeleo kama vile Ujenzi wa barabara
na miradi mingine mikubwa ya kitaifa.
Washiriki wa mkutano huo walisema Benki za
kiislamu zinafanyakazi katika uchumi
halisi kwa kuzingztia uadili na ukweli hali inayopelekea watumiaji wa huduma hiyo kuweza
kukuza mitaji yao bilaya kuingia kwenye Riba ambayo imeharamishwa katika uislamu.
Walisema
mifumo ya Benki za kiislamu miongoni mwa faida zake ni kupunguza mfumuko wa bei, kukuza nafasi za ajira na kuzalisha bidhaa ambazo
zinahitajika katika matumizi ya binadamu
kwani kwa kutumia mfumo wa kiislamu kunazingatiwa mahitaji muhimu ya kijamii katika uwekezaji na hivyo
hata matumiziya fedhayanalenga
katika mahitaji hali ya mwananchi
wa kawaida.
Aidha, walisema athari zinazotokana na Riba
zinaonekana hata katika nchi kwa
kuongezeka madeni ya nje ambayo misingi yake niRiba hivyo ni wazi kuwa ikiwa
kama nchiinaweza kutetereka kutokana na
riba kwenye mikopo
basi kwa mwananchi wa kawaida pia mfumo huu
utamuathiri zaidi.
Walisema uislamu
umeharamisha Riba na umehalalisha Biashara hivyo katika mfumo wa kiislamu fesa sio bidhaa
hivyo mwenye kukopesha fedha anapaswa kurudishiwa kiasi kilekile lakini ikiwa anataka faida
basi uislamu umeruhusu kufanya biashara
ili upate faida.
UELEWA MDOGO MIONGONI MWA JAMII
Katika kuwasilisha mada, washiriki waliweza kutaja miongoni mwa changamoto zinazoikabili Benki za
Kiislamu katikanchi za Afrikani pamoja uelewa mdogo miongoni mwa jamii.
Akizungumzia hilo, Mkurugenzi wa Amana Bank, Dkt. Muhsin
Masoud alisema Tanzania kwa sasa inafika miaka tisa toka kuwepo kwa Benki za kiislamu lakinibado kuna watu hawaelewi mfumo wa Benki
za kiislamu.
Alisema wapo
wanodhani kuwa watumiaji wa Benki
hizo ni waislamu
pekee jambo ambalo siosahihi
lakini pia bado kwa
waislamu kunahitajikakuongeza
uelewa ili kutofautisha Benki
zinazotumia mifumo ya Riba na
Benki ambazo hazitumii mifumo ya Riba.
Alisema Elimu
inahitajika ili kuifahamisha
jamii,nini hasa maana Riba, Madhara
yake, na namna ya kuiepuka ili jamii iondokane na miamala inayoambatana na Riba.
Mkutano huo
wa siku mbili wa kujadili Uchumi
wa Kiislamu Afrika umeandaliwa na Shirika
la Kimataifa la Alhuda Centeter of Islamic
Banking and Economics (CIBE) lenye makao yake makuu nchini Dubai, uliolenga kuwasilisha Changamoto za kiuchumi na kufungua milango kwa wawekezaji kutoka nje
ya Afrika.
umehudhuriwa
na nchi kumi zaidi ya kumi ambapo kwa pamoja
wamekubaliana kuongeza Elimu juu
ya matumizi ya Benki za
kiislamu, Uharamu wa Riba na kuzitaka
Serikali za nchi za Afrika
kutunga Sheria zitakazosimamia uendeshaji
wa Benki za Kiislamu.
No comments:
Post a Comment