DC NICKSON SIMON: USHIRIKIANO WA SERIKALI NA NGOs NI NGUZO YA MAENDELEO YA WANANCHI
KIBAHA – Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon, amezitaka Asasi Zisizo za Kiserikali (NGOs) wilayani humo kuimarisha ushirikiano na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuongeza tija na kuleta matokeo chanya kwa wananchi. Akifungua kikao cha mashauriano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na wawakilishi wa NGOs kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, DC. Nickson alisema Serikali na NGOs zina lengo moja la kuwaletea wananchi maendeleo, hivyo ni muhimu shughuli na miradi inayotekelezwa iwe na mshikamano na kuendana na vipaumbele vya taifa. Alieleza kuwa ushirikiano huo unaonekana katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ambapo Serikali na NGOs zote zinatekeleza miradi ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Aliongeza kuwa hali hiyo pia ipo katika sekta za afya, mazingira, haki za binadamu pamoja na uwezeshaji wa makundi maalumu. Katika kikao hicho, Mkuu wa Wilaya aliainisha maeneo muhimu yanayopaswa kupewa kipaumbele na NGOs kwa kuzi...