Posts

TUSIKIMBIE KUFANYA KAZI VIJIJINI - KIKWETE

Image
  Watumishi wa Serikali wametakiwa kuacha tabia ya kukimbia kufanya kazi sehemu wanazopangiwa na kuchagua sehemu wanazotaka wao. Maneno hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Ndg. Ridhiwani Kikwete alipokuwa anazungumza na watumishi wa Halmashauri ya Chalinze katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo. Ndg. Kikwete alitumia mkutano huo kuwakumbusha watumishi umuhimu wa kufanya kazi kuzingatia misingi ya kazi ikiwemo kujitambua na kutambua tunaowahudumia.  Katika kusistiza utumishi wenye tija na weledi, Naibu Waziri huyo aliwakumbusha watumishi kuendelea kuwahudumia wananchi wote sawa na hakuna sababu ya kuchagua na kuweka madaraja katika utoaji wa huduma.  Katika mkutano huo , Ndg. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha umuhimu wa kutochagua vituo vya kazi huku akiwakumbusha kuwa uchaguzi wa Vituo vya kazi unalenga sio tu kuwasaidia baadhi lakini unatengeneza madaraja katika utumishi wa umma.  Aidha, Kikwete alitumia n...

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 29 SEPTEMBA 2023.

Image
 

MAJALIWA: VIONGOZI WA DINI TUSHIRIKIANE KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA

Image
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa madhehebu ya mbalimbali ya dini nchini waendelee kushirikiana na Serikali katika kupiga vita biashara na matumizi ya dawa za kulevya .    "Tushirikiane kupambana na biashara na matumizi ya dawa za kulevya ambayo yameathiri zaidi vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa."    Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Alhamisi, Septemba 28, 2023), alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Baraza la Maulid lililofanyika Kitaifa jijini Dodoma kwenye kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete.   “Matumizi ya dawa za kulevya yana madhara mengi kwa Taifa yakiwemo ya kiuchumi, kiafya na kimazingira pamoja na kuathiri uwezo wa mtu kufikiri”   Pia, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi wa dini waendelee kukemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii na wawahamasishe waumini kushiriki katika shughuli zitakazowaongezea kipato.    Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka wananchi waendelee kudu...

MAGAZETI YA LEO TAREHE 28 SEPTEMBA 2023.

Image