KINONDONI YA SAINI MKATABA NA JWTZ UJENZI WA UWANJA WA KISASA, JENGO LA UTAWALA, MEYA SITTA ASEMA MKURUGENZI KAGURUMJULI NI MSIKIVU.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta katikati mwenyesuti, akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mahudu Kazi wa kwanza kulia, Luteni Kanali wa JWTZ David Luoga wakipitia nyaraka za mkataba wa ujenzi wa Jengo la Utawala pamoja na Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu. Luteni Kanali wa JWTZ David Luoga, akiwaonyesha Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Benjamini Sitta, Kaimu Mkurugenzi Mahudu Kazi, mchoro wa uwanja wa mpira wa miguu utakavyokuwa. Mwenye shati la kijani kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Mhe. Harlod Muruma. Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta mwenyesuti akipeana mkono na Luteni Kanali David Luoga wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kusaini mkataba na ujenzi wa miradi miwili mikubwa ya Jengo la Utawala pamoja na Uwanja wa mpira wa miguu. ................................... Halmashauri ...