Posts

MAGAZETI YALEO MEI 27, 2019.

Image

AMANA BANK, VODACOM WAZINDUA HUDUMA MPYA YA HALAL PESA.

Image
Amana Bank kwa kushirikiana na Mtandao wa simu za mkononi wa Vodacom kwa pamoja wamezindua huduma mpya ijulikanayo kama ''halal pesa''. Huduma hii mpya sasa itapatikana kwa wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa na wale wa Amana Bank kwa kuzingatia misngi ya sheria ya kiislamu. Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi mtendaji wa Amana Bank, Dkt. Muhsin Salim Masoud, alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakifikiria jinsi ya kuwafikia wateja wengi zaidi ambao wanapenda kutumia miamala ya kifedha kwa mujibu wa sheria ya kiislamu. Dkt. Muhsin alisema Amana Bank imekuwa ikibuni njia mbalimbali za kuwafikia wateja wake wazamani na wapya hivyo wameweza kuanzisha huduma hiyo ya halal pesa ambapo wateja wa Vodacom wanaotumia M-pesa wataipata huduma hiyo mpya inayozingatia misingi ya sheria ya kiislamu. Alisema katika huduma ya halal pesa mteja wa Amana Bank anaweza kufanya miamala yake kwa kutumia Vodaco M-Pesa huku akiwa bado yupo kwenye s...

MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI KATIKA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI WAZINDULIWA.

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (katikati) akiwa tayari kukata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua  Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Vijiji, Wilaya na Mikoa itakayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) wa tatu kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry  aliyeshika kipaza sauti. ......................................  Serikali imezindua Mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa Vijiji, Wilaya na Mikoa itakayopitiwa na mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ikiwa ni hatua nyingine katika utekelezaji wa mradi huo. Mpango huo umezinduliwa katika Kijiji cha Sojo, Kata ya Igusule, wilayani Nzega, Mkoa wa Tabora tarehe 25/5/2019 na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliye ambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanry na Meneja Mradi wa EACOP, Mantin Tiff...