MADEREVA DAR-BAGAMOYO WALALAMIKIA KITUO CHA TEGETA NYUKI.
Wamiliki na madereva wa mabasi yanayofanya safari Dar-Bagamoyo wamelalamikia miundombinu ya kituo cha Tegeta Nyuki kuwa sio mizuri kwa kuingiza magari kituoni hapo. Wakizungumza na wanaadishi wa Habari kituoni hapo, Madereva hao walisema kituo hicho hakijaandaliwa kwa matumizi ya mabasi mengi, na kwamba kuhamishia mabasi ya Bagamoyo kituoni hapo ni kuleta usumbufu. Wakitaja baadhi ya mapungufu yaliyopo katika kituo hicho walisema ni pamoja na ubovu wa eneo lote la kituo kwakuwa limechimbika na kusababisha mashimo yanaopelekea kujaa maji wakati wa mvua na kusababisha usumbufu kwa abiria na magari yanayoingi humo. Aidha, walisema Geti la kuingilia magari kuna shimo kubwa linalosababisha magari kukwama wakati wa kuingia, kukosekana kwa taa usiku uchache wa vyoo pamoja na udogo wa eneo leneyewe la kituo hicho. Malalamiko ya madereva hao yamekuja kufuatia amri ya kuwataka kuondoka katika kituo cha makubusho na kuwataka kuishia kituo cha Tegeta nyuki. Katika Barua ...