Posts

MV NJOMBE NA MV RUVUMA, ZAKAMILIKA MKOANI MBEYA.

Image
Meli mbili za Mv. Ruvuma na Mv Njombe zikiwa katika cherezo katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, zikiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio ndani ya Ziwa Nyasa Mwishoni mwa Februari, 2017.   Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mchoro wa meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja anazoziunda kwa ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na ujumbe wa Serikali unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani Mbeya. ................................. UJENZI wa meli mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani Mbeya, MV Njombe na MV Ruvuma, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 na kwamba meli hizo zinatarajiwa kufanyiwa majaribio Ziwa Nyasa, mwishoni mwa mwezi Februari na kukabidhiwa rasmi Serikalini mwezi Machi, 2017. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Mar...