Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kongamano la vijana katika kilimo lililofanyika Njombe na
kukutanisha vijana 200 toka mikoa ya Njimbe ,Iringa na Ruvuma jana.
.......................................
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba
ameziagiza halmashauri zote nchini kutenga ardhi ya kutosha kwa ajili ya vijana
kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi .
Ametoa agizo hilo mjini Njombe
wakati alipofungua kongamano la vijana wa mikoa ya Njombe,Ruvuma na Iringa
kujadili fursa zilizopo katika sekta ya kilimo nchini.
Mgumba amesema kumekupo na malalamiko
ya vijana kukosa ardhi kutokana na halmashauri kuwa na mashamba pori mengi
yasiyopimwa na kulimwa.
“Halmasahauri zote zihakiki mashamba
pori yote au yaliyochukuliwa mikopo na hayalimwi yapimwe na kugawiwa kwa vijana
walio tayari kufanya kazi za kilimo nchini”.alisema Naibu Waziri Mgumba.
Ili kufanikisha hilo Mgumba mewataka
vijana kujisajili kwenye daftari la wakulima linaroratibiwa na wizara yake ili
serikali iwatambue na kujua changamoto zao na kisha kuwaonyesha
fursa za ajira kwenye kilimo.
Naibu Waziri Mgumba amesisitiza
halmashauri nchini kutoa fedha za mikopo kwa vijana bila urasimu ili vijana
wanufaike na kuanzisha kazi za uzalishaji mazao ya kilimo na mifugo.
Mgumba aliwafahamisha kuwa serikali
imeelekeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) kuendelea kutoa mikopo kwa
vijana ili wapate mitaji.
“Wapo vijana wengi wasomi wameamua
kujiajili katika kilimo ili kufikia malengo ya kuongeza ajira ikiwa ni malengo
ya Serikali ya Awamu ya Tano kukuza sekta ya kilimo” alisema Mgumba.
Tanzania ina eneo la hekta milioni 44
zinazofaa kwa kilimo hivyo vijana wajitokeze kutumia fursa hiyo kuanzisha kazi
za kuzalisha mazao ya kilimo .
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Njombe Ruth Msafiri aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe aliziagiza
halmashauri zote za mkoa wa Njombe kuandaa katiba kwa
ajili vijana
kushiriki shughuli za kilimo.
Aliongeza kusema watendaji wote wa
halmashauri wapunguze urasimu kwa kukaa muda mrefu bila kupitisha maombi ya
vijana wanaostahili mikopo ya fedha za mapato
ya ndani.
“Halmashauri punguzeni urasimu msikae
zaidi ya robo mwaka bila kutoa mikopo kwa vijana,akina mama na walemavu”
alisema Mkuu huyo wa wilaya ya Njombe.
Naye Mkurugezi wa Shirika la SUGECO
Revocatus Kimario linaloratibu mafunzo maalum kwa vijana kwenda Israel na
Marekani kujifunza fursa za kilimo kwa vitendo kwa mwaka mmoja amesema wengi
wamenufaika.
Kimario amesema hadi sasa zaidi ya
vijana 1000 wamepatiwa mafunzo ya kilimo,mifugo na uvuvi nchini Israel na
wengine 90 nchini Marekani wamerudi nyumbani
wamefanikiwa
kuzalisha ajira nyingi kwa wenzao .
Kimario ameishauri jamii kutotumia
kilimo kama adhabu bali kitumike kama fursa ya kukuza ajira na kipato cha kaya
na taifa.
Kongamano hilo la siku mbili
linawakutanisha vijana wapatao mia mbili toka mikoa ya Njombe,Ruvuma na Iringa
chini ya uratibu wa Wizara ya Kilimo na wadau toka wizara za kisekta na taasisi
binafsi.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kongamano la vijana katika kilimo linalofanyika Njombe na
kukutanisha vijana 200 toka mikoa ya Njimbe ,Iringa na Ruvuma jana.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akisikiliza
maelezo ya jinsi ya kuzalisha bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo toka kwa
kijana mjasiliamali Fatuma Mbaga (kushoto) toka Shirika la SUGECO la
Morogoro.
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kongamano la vijana katika kilimo linalofanyika Njombe na
kukutanisha vijana 200 toka mikoa ya Njimbe ,Iringa na Ruvuma jana.