Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa kiwanda cha sabuni cha KEDS wilayani Kibaha, Bw. Jack Feni (Kushoto
kwake) kuhushu mitambo ya kiwanda hicho hicho
wakati alipokitembela September 19, 2017. Kulia kwake ni. Mkuu wa
Mkoa wa Pwani, Mahandisi Evarest Ndikilo na kulia ni Mbunge wa Kibaha Mjini,
Silyvestry Koka.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
........................................
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Pwani waboreshe
miundombinu ya maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ili waweze
kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani.
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne, Septemba 19, 2017) wakati akizungumza na
kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga
cha Keds kilichopo Kibaha na kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford
kilichopo Chalinze.
Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa
viwanda mkoani Pwani na amewaagiza viongozi wahakikishe maeneo yaliyotengwa kwa
ajili ya uwekezaji yanakuwa na miundombinu muhimu kama maji, umeme na barabara.
“Nimefarijika kuona miradi hii mikubwa ya ujenzi wa viwanda ikiwa katika
hatua za mwisho kukamilika, nawashukuru kwa kuunga mkono mkakati wa Rais Dkt.
John Magufuli wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.”
Amesema mbali na viwanda hivyo kutoa ajira nyingi kwa Watanzania, pia
vitakapoanza uzalishaji vitawawezesha wananchi kupata bidhaa mbalimbali kama
vigae kwa bei nafuu kwa kuwa vitakuwa vinazalishwa nchini.
Pia Waziri Mkuu amewataka wananchi wanaofanyakazi kwenye viwanda hivyo
wawe mabalozi wazuri wa Taifa kwa kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa
ili kuwathibitishia wawekezaji kwamba wao wanauwezo mkubwa wa kufanya kazi na
hakuna haja ya kutafuta wafanyakazi kutoka nje ya nchi.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa viwanda hivyo Bw. Jack Feng amesema ujenzi
wa huo umekamilika kwa asilimia 90 na sasa wako katika hatua za mwisho ikiwa ni
pamoja na ufungaji wa mitambo na vinatarajiwa kuanza uzalishaji Oktoba mwaka
huu.
Amesema vigae watavyovizalisha wanatarajia kuviuza kwa gharama nafuu kwa
sababu asilimia 95 ya malighafi inapatikana ndani ya nchi. Pia ameahidi kutoa
ajira nyingi kwa wananchi waishio kwenye maeneo yanayozunguka viwanda hivyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo
amemuomba Waziri Mkuu awasaidie upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha
kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.
Mhandisi Ndikilo amesema mahitaji waliyonayo ya nishati ya umeme ni
megawati 92, ambapo kwa sasa wanasambaziwa megawati 40, hivyo ameomba suala
hilo lipatiwe ufumbuzi wa haraka ili lisije kuathiri uzalishaji.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, SEPTEMBA 19, 2017.
No comments:
Post a Comment