Wazazi na walezi wa kiislmu wametakiwa kuendelea
kuwasomesha elimu ya dini ya kiislamu watoto wao hata baada ya kumaliza elimu
ya msingi ili kuwajengea misingi ya kumjua Mwenyezimungu katika maisha yao
yote.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya The
Islamic Foundation (TIF) Aref Nahd alipokuwa akizungumza katika mahafali ya 06
ya kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba 2017 wa shule ya msingi Yemeni English
Medium Primary School iliyopo Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Aref, alisema imekuwa ni kawaida ya wazazi na
walezi wengi kuwakatisha masomo ya elimu ya dini kiislamu watoto wao mara watoto hao wanapomaliza Elimu ya msingi
jambo ambalo linawafanya watoto kutoka kwenye misingi ya uislamu kwasababu
hawakuendelezwa kwenye Elimu ya uislamu na badala yake wameendelezwa kwenye
Elimu ya mazingira pekee.
Alisema uislamu ni dini iliyobeba maisha ya
binadamu kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufa kwake hivyo muislamu hana nafasi ya
kuishi nje ya mfumo ulioelekezwa na uislamu.
Aliongeza kwa kusema kuwa, mfumo huo wa maisha ya
binadamu umefundishwa ndani ya uislamu kupitia Mtume Muhammad Swalallahu Alayhi
Waslama, na kwamba huwezi kujua bila ya kusoma Elimu ya dini ya uislamu.
Alisema si vyema kwa mzazi au mlezi kumkatisha
masomo ya elimu ya uislamu mtoto kwasababu mtoto huyo anaendelea kukua na bado
anahitaji muongozo kutoka katika Qur'ani na sunnah ambavyo ndio dira ya maisha
yake itakayompatia faida duniani na akhera.
Aidha, Aref Nahdi ambae ndiye aliyekuwa Mgeni
rasmi katika Mahafali hayo aliwataka vijana walimaliza elimu ya msingi shuleni
hapo kuendelea kuwa na tabia njema ya kiislamu kama walivyofundishwa wakiwa
shuleni na kwamba wanapaswa kutambua kuwa, kumaliza elimu ya msingi sio mwisho
wa kutafuta elimu katika maisha.
Wakati huo huo Aref aliwataka walimu kufanya kazi
kwa moyo mmoja wakitambua kuwa kazi yao ni miongoni mwa sadaka licha ya kuwa
wanalipwa mishahara.
Alisema pamoja na kufikiria kuongezwa posho na
mishahara wanapaswa pia kufikiria mbinu mbalimbali za kuongeza taaluma ili
watoto wanaoletwa katika shule hiyo wapate elimu bora kama ilivyokusudiwa.
Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya The Islamic
Foundation (TIF) inayomiliki vyombo vya habari vya Tvimaan, Radio imaan, pamoja na Gazeti imaan,
ametoa nafasi kwa uongozi wa shule hiyo ya Yemen English Midium Primary school
kufika katika studio za Tvimaan zilizopo mjini Morogoro kuitangaza shule hiyo
bure kwa kueleza namna wanavyoendesha shule hiyo ili watu wengi wajue Taaluma
inayotolewa shuleni hapo.
Alisema
The Islamic Foundation inatoa nafasi hiyo ya muda wa hewani bure kupitia
Tvimaan ikiwa kama ni mchango wake kwa shule hiyo ambapo kipindi hicho kama
kingelipiwa kinagharimu shilingi milioni tatu.
Aidha, alisema pamoja na muda huo wa hewani
kupitia Tvimaan, TIF itatoa nakala ishirini za gazeti imaan shuleni hapo kila
wiki ili walimu kupitia Gazeti hilo
waweze kufaidika na taaluma inayotolewa ndani gazeti hilo na kuwajenga vijana
wa kiislamu wanaosoma shule kuanza kupenda vyombo vyao vya habari kuanzia
shuleni.
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Hassan Akrabi, aliwataka wazazi wote wenye
watoto waliomaliza elimu ya msingi shuleni hapo kuwarudisha tena katika shule
hiyo kuendelea na masomo ya Sekondari ili waendelee kupat malezi yenye maadili
pamoja na elimu bora inayotolewa katika shule hiyo.
Alisema watoto hao wamejengwa katika misingi ya
kumjua Mwenyezimungu na kupata Elimu bora ya muongozo na mazingira hivyo
uongozi wa shule unaomba ridhaa ya kubaki tena na watoto hao kuanzia kidato cha
kwanza mpka cha nne.
Mwenyekiti huyo wa bodi ya shule alisema kumjenga
mtoto kitabia inachukua muda mrefu na juhudi za ziada lakini kumbomoa inachukua
muda mfupi na kwamba wazazi wasipokuwa makini kuchagua shule za kuwapeleka
watoto wao watawabomoa kimaadili na kitaaluma.
Mbunge wa viti maalum Da es
salaam Zainabu Mndolwa Amiri akizungumza katika mahafali hayo katikati ni Mjumbe wa kamati ya shule Dkt. Tausi Mftaha na kushoto ni meneja wa shule hiyo Jamila Awadhi.
Mbunge wa viti maalum Da es
salaam Zainabu Mndolwa Amiri akimkabidhi mwanafunzi cheti pamoja na Dictionary, ambapo watoto wote mia moja na moja 101 kila mmoja alipata Dictionary moja
katika mahafali hayo, katikati ni Mjumbe wa kamati ya shule Dkt. Tausi
Mftaha na kushoto ni meneja wa shule hiyo Jamila Awadhi.
Kwa upande wake Mbunge wa viti maalum Da es
salaam Zainabu Mndolwa Amiri amejitolea
Dictionary 102 ambapo kila muhitimu alipata Dictionary
Mbunge huyo alisema amejitolea Dictionary hizo
ili kuunga mkono juhudi za kuwawezesha vijana kielimu na kuwataka vijana hao
waongeze bidii katika safari yao ya masomo.
Dictionary hizo aina ya Oxford zimegharimu
shilingi za kitanznia milion moja laki tatu elfu arubaini na sita na mia nne,
1,346,400/= ambapo kila moj ina thamani ya shilingi elfu kumi na tatu na mia
mbili, 13,200/=
Aidha, aliupongeza uongozi wa Yemeni English
Medium Primary School kwa kuisimmia vizuri shule hiyo na kufanikiwa kutoa
watoto wenye maadili ambao watakuwa na faida kwa wazazi wao na taifa kwa
ujumla.
Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rahim Burhan
Abdallaah, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hza Yemen, Hassan Akrabi, na watatu ni Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti, wa the islamic Foundation, Aref Nahdi.
Awali
akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Rahim Burhan
Abdallaah alisem miongoni mwa mafanikio yalipatikana shuleni hapo ni pamoja na
kukamilika kwa jengo la ghorofa tatu ambalo lina jumuisha Madarasa 36, Ofisi
18, Vyoo 52 Stoo 02, Maktaba 01, Chumba cha Mabara 01 Maabara ya Computer 01 na
Ukumbi wa mikutano 01.
Aidha, alisema wanafunzi wameongezeka kutoka 35
Mwaka 1999 na kufikia 807 Mwaka 2017 na walimu kutoka walimu watatu mwaka 1999
mpaka walimu 48 mwaka 2017 huku shule ikiwa inamiliki mabasi manne kwaajili ya
kusafirishia wanafunzi.
Alisema pamoja na mafanikio hayo, miongoni mwa
Changamoto zinazoikabili shule hiyo ni pamoja na uhba wa mabasi ya kusafirisha
wanafunzi na kuwataka wadau mbalimbali kujitokeza kutoa huduma ya usafiri
shuleni hapo kwa gharama nafuu.
Aidha, alisema malengo ya shule hiyo ili kuendana
na uwezo wa shule, ni kufikia wanafunzi elfu moja mia mbili na tano 1,205,
kutoka wanafunzi mia nane na saba 807, waliopo sasa.
Jumla ya vijana mia moja na moja 101, wamehitimu Elimu ya
msingi shuleni hapo wakiwemo wavulana 44 na wasichana 57 .
Muonekano wa majengo katika shule hiyo ya Yemen English Medium Primary School iliyopo Chang'ombe jijini dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa elimu ya msingi wasichana 2017.
Baadhi ya wahitimu wa elimu ya msingi wavulana 2017.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, ambae ni mwenyekiti wa The Islamic Foundation, Aref Nahdi (katikati) Kulia ni mwenyekiti wa Bodi ya shule za yemen, Hassan Akrabi, na kushoto ni Mjumbe wa bodi ya shule za yemen Salmeen Aljabry.
Wa kwanza kulia ni Mbunge wa viti maalum Dar es Salaam, Mh. Zainab Mndolwa Amiri, katikati ni mjumbe wa kamati ya wazazi wa shule hiyo, Dkt. Tausi Maftah, na wa kwanza kushoto ni Meneja wa shule hiyo, Jamila Awadhi.
No comments:
Post a Comment