WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ,Angella Kairuki ,akizungumza wakati wa mkutano na watumishi wa
halmashauri ya Kibaha Mjini na Vijijini pamoja na watumishi wa mkoa wa Pwani
kufuatilia zoezi la uhakiki wa vyeti namna lilivyofanyika kwenye mkoa huo,wa
kwanza kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo .
...................
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora ,Angella Kairuki ametaka ,mshahara wa katibu tawala msaidizi uratibu wa
serikali za mitaa sekretarieti ya mkoa wa Pwani ,Martha Nzungu,uondolewe kwenye
mfumo wa malipo baada ya kuhakikiwa cheti chake kidato cha nne chenye majina
tofauti.
Aidha ametoa rai,watumishi wa umma nchini wanaotumia vyeti vya kughushi
ama visivyo vyao wajiondoe wenyewe mara moja katika utumishi wa umma kwani
wakiendelea kukaa itawagharimu .
Kairuki ameeleza ,endapo atabainika mtumishi cheti cha magumashi
atatakiwa kurejesha mishahara ya miezi yote aliyoiibia serikali.
Aliyasema hayo mjini Kibaha wakati wa mkutano na watumishi wa halmashauri
za Kibaha Mjini na Vijijini pamoja na watumishi wa mkoa wa Pwani kufuatilia
zoezi la uhakiki wa vyeti lilivyofanyika kwenye mkoa huo.
Alieleza mtumishi huyo anapaswa kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mshahara
ili kupisha uchunguzi.
Kairuki alieleza,kuna kila sababu ya kufanya uchunguzi juu ya suala lake
la kutumia majina tofauti ya kwenye malipo ya mshahara na jina la kwenye cheti
chake.
Alisema cheti chake cha kidato cha nne kipelekwe baraza la mitihani NECTA
kwa ajili ya kuhakikiwa .
Hata hivyo Kairuki alipongeza, hatua ya kusimamishwa kwa Martha
Nzungu kutokana na kushindwa kuwasilisha vyeti vya kitaaluma tangu Julai mwaka
huu.
“jitihada zinazoendelea za uhakiki wa watumishi wa umma
bado zoezi hilo limekuwa na dosari kwani kuna baadhi bado wanaendelea kutumia
vyeti visivyo vyao,” alisema Kairuki.
“Makatibu tawala wa mikoa wanapaswa kuangalia na kujiridhisha na majina
ya watumishi kwenye orodha ya malipo ya mishahara ya watumishi wa umma na ya
kwenye zoezi la uhakiki kama yanafanana”
“Majina yalioonekana kwenye zoezi la uhakiki ndiyo yanayopaswa kuonekana
kwenye orodha ya malipo ya mishahara na kama kuna mtumishi hajahakikiwa
anatakiwa aondolewe kwenye malipo ya mshahara,” alifafanua Kairuki.
Nae mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo alisema mkoa ulifanya
zoezi hilo kama serikali ilivyoelekeza ili kubaki na watumishi wenye sifa na
kuwaondoa wale wasio na sifa.
Mhandisi Ndikilo alieleza ,watumishi waliopewa dhamana ya kusimamia mfumo
huo wa kuhakiki watumishi wasifanye kazi hiyo kwa kulindana ili kuepuka
kuendelea kuwa na watumishi wasio na sifa.
Hivi karibuni ,Martha Nzungu ambae pia ni mke wa katibu tawala
(RAS)mstaafu mkoa wa Pwani ,Bernard Nzungu alitakiwa kuwasilisha vyeti vya
kitaaluma kwani jina analotambulika kwenye malipo ni tofauti na lililopo kwenye
vyeti
No comments:
Post a Comment