Monday, September 25, 2017

WAZIRI WA AFYA AWEKA JIWE LA MSINGI BAGAMOYO.


Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, katikati akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi jengo la wagonjwa wa dharula, katika Hospitli ya wilaya ya Bagamoyo, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Taasisi ya kiislamu ya Dhi Nureyn, Sheikh Saidi Abry ambao ndio wafadhili wa ujenzi huo na kushoto kwake ni Mfadhili mwenza kutoka Saudi Arabia, Sheikh Saleh Abdulazizi, wa kwanza kulia mwenye kofia ya njano ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj majid mwanga, wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya bagamoyo, Dkt. Sylivia Mamkwe, wa pili kushoto ni Mbunge wa jimbo la bagamoyo, Dkt. shukuru Kawambwa, na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Aliy Aliy.
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameweka mawe ya msingi majengo mawili katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.

Majengo hayo mawili ni jengo la wagonjwa wa dharula na jengo la wodi ya wazazi ambayo yote yanajengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Dhi Nureyn yenye makao yake makuu mjini Iringa ikishirikiana na wahisani kutoka nchini Saudi Arabia.
Muonekano wa jengo la wagonjwa wa dharula.
  Muonekano wa jengo la wodi ya wazazi.
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, (katikati) akimsikiliza mfadhili wa majengo hayo kutoka nchini Saudi Arabia, Sheikh Saleh Abdulazizi,(kulia) kushoto kwa waziri ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Sylivia Mamkwe, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaji, Majid Mwanga, wa pili kushoto ni daktari mshauri wa Taasisi ya dhi nureyn, Dkt. Swaleh, na wa tatu kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi nureyn ambayo ndiyo iliyofadhili majengo hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj majid Mwanga, kulia akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na wa katikati ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Sylivia Mamkwe, wakiwa ndani ya jengo la wagonjwa wa dharula linaloendelea kujengwa, wakati wakimsubiri Waziri wa Afya kuweka mawe ya msingi katika majengo ya wagonjwa wa dharula na wodi ya wazazi yanayojengwa kwa ufadhili wa Dhi nureyn wakishirikiana na wahisani kutoka Saudi arabia.

Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa akimsikiliza mfadhili wa majengo hayo Sheikh Saleh Abdulazizi (kulia) na wa katikati ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Sylivia Mamkwe wakiwa ndani ya jengo la wodi ya wazazi.

Kulia ni Mhandisi wa Majengo hayo majengo hayo kutoka Taasisi ya Dhi Nureyn Ally Upete.

No comments:

Post a Comment