Naibu
Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha,mwenye shati la draft akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ruvu, (CHAURU)Sadala Chacha, (kushoto), Kulia mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, majid Mwanga, wakati naibu waziri huyo alipotembelea mashamba ya kilimo cha umwagiliaji cha mpunga Ruvu jana Tarehe 29 Septemba 2017.
Naibu Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha,mwenye shati la draft akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Ruvu, (CHAURU)Sadala Chacha, (kushoto), Kushoto kwa Naibu waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, majid Mwanga, na wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, wakati Naibu waziri huyo alipotembelea mashamba ya kilimo cha umwagiliaji cha mpunga Ruvu jana Tarehe 29 Septemba 2017.
..........................
Naibu Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate
Wiliamu Ole nasha, amemtaka muwekezaji wa raia wa China Guo Ming Tang kuacha kuwakodisha mashamba wanachama wa
Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU) ili wanachama hao wafaidike na mashamba hayo
ambayo yameandaliwa na Serikali kwaajili ya wananchi.
Kauli hiyo ya naibu waziri huyo mwenye dhamana ya
kilimo, Mifugo na Uvuvi ameitoa katika
mashamba ya ushirika ya Chama cha Ushirika Ruvu (CHAURU) yaliyopo Ruvu katika
Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Alisema pamoja na kuacha kuwakodisha mashamba
wananchi pia muwekezaji huyo ametakiwa kuacha tabia ya kuwauzia wananchi
wanachama wa CHAURU maji kwaajili kumwagilia katika mashamba hayo.
Aidha, alimtaka muwekezaji huyo kufungulia mitaro
ya maji yanayoingia mashambani ambayo aliifunga kwa lengo la kuuza maji hayo
kwa wakulima na kusema kuwa ni marufuku kuzuia maji hayo ambayo miundombinu
yake imetengezwa na serikali kwaajili ya wakulima wa mashamba hayo.
Awali akitoa taarifa mbele ya naibu waziri
Mwenyekiti wa Chama cha ushirika Ruvu (CHAURU) Sadala Chacha alisema wanaiomba
wizara kuingilia kati Mgogoro wa muda mrefu baina ya mwekezaji huyo raia wa
China na wakulima hali inyopelekea wakulima kukosa haki zao za msingi kama
wanachama huku wakitishiwa usalama wao na wengine kupigwa.
Alisema muwekezaji huyo aliingia mkataba kinyume
cha sheria mwaka 2012 na mwenyekiti wa
CHAURU (wakati huo) ambapo katika mkatba
huo kampuni hiyo ya Guo ming Tang imekabidhiwa ekari 354 za shamba la
umwagiliaji lakilimo cha mpunga.
Aidh, pamoja na kukabidhiwa kinyume cha sheria
shamba hilo muwekezaji huyo hana uwezo wa kulima shamba lote hilo na badala
yake zaidi ya heka 300 anazikodisha kwa wananchi kinyume cha sheria na yeye
hulima heka 50 tu.
Akifafanua mazingirz ya mkatba huo Sadala alisema
Mkataba huo una mazingirz ya rushwa kwakuwa mkataba huo umetiwa saini na mtu
mmoja tu jambo ambalo ni kinyume cha sheria na masharti ya vyama vya ushirika
nchini na kwamba mkataba huo haukujadiliwa na Bodi ya CHAURU wala kupitishwa kwenye
mkutano mkuu.
Aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na kuziba
mfereji wa maji unaopeleka maji kwenye shamba namba 11, kumepelekea ekari 24 kutolimika
kwa kipindi cha miaka 5 sasa na kusababisha upotevu wa wastan wa kilo 236,000
za mpunga zenye thamani ya shilingi milioni mia mbili na laki sita,
200,600,000/=
Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ole nasha,
amemuagiza Mrajisi wa Mkoa wa Pwani kukaa na muwekezaji huyo ili kupitia upya
mkataba huo na kama masharti ya mkataba yamekiukwa hatua za haraka zichukuliwe
ili wanachama wa CHAURU wabaki katika mazingira salama ya kufanya shughuli zao
za kilimo kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Chama cha Ushirika Ruvu kimeanzishwa mwaka 2002 kikiwa
na wanachama 350 wanaofanya shughuli za za kulima mpunga katika eneo la Ruvu na
mpaka sasa kuna wanachama 894 ambao
wanalima katika shmba hilo lenye ukubwa wa hekta 720.
Mwenyekiti
wa CHAURU Sadala Chacha alisema katika
msimu wa kilimo wa mwaka 2015/2016 kimefanikiwa kuzalisha mpunga tani 5.6 kwa
kulima hekta 497.4 ambapo msimu wa mwaka 2016/2017. wamefanikiwa kuvuna tani
5.0 kwa kulima hekta 565.6
Sadala alisema katika msimu wa kilimo 2017/2018
wanatarajia kulima hekta 640 na kuvuna tani 7.0
Muwekezaji raia wa China, Guo Ming Tang kwenye Mashamba ya Mpunga CHAURU, akisikiliza kwa makini maelekezo ya Naibu Waziri wa kilimo, mifugo na Uvuvi.
Naibu
Waziri wa kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Tate Wiliamu Ole nasha akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Ruvu, (CHAURU) Chacha Sadala, katika eneo la mashamba ya mpunga Ruvu, wilayani Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Ushirika Ruvu, (CHAURU) Chacha Sadala,akimunesha Naibu waziri miundombinu iliyharibiwa na muwekezaji raia wa China aliyokodishwa ekari 354 katika eneo la mashamba ya mpunga Ruvu, wilayani Bagamoyo, wakati naibu waziri huyo alipotembelea eneo hilo.
Mkuu wa
Wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, majid Mwanga,(aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi mara alipowasili katika ofisi za CHAURU Ruvu
No comments:
Post a Comment