Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto)
akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Tanzania wakati wa maadhimisho ya siku ya
87 ya Taifa la Kifalme la Saudi Arabia yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Prof. Maghembe alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kulia ni Balozi wa
taifa hilo nchini Tanzania, Balozi Mohammed Bin Mansour Al Malik.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne
Maghembe (katikati), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour
Al Malik (wa pili kulia) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakijiandaa kukata
keki ya maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (wa tatu
kushoto), Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mohammed Bin Mansour Al Malik
(katikati) na viongozi wengine wa ubalozi huo wakikata keki ya maadhimisho
hayo.
Baadhi ya watoto wa Taifa la Kifalme la Saudi Arabia wakiinua bendera
ya nchi hiyo kuashiria maadhimisho ya siku ya 87 ya Taifa hilo
yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment