Tuesday, September 26, 2017

SERIKALI YATAMBUA MCHANGO WA DHI NUREYN BAGAMOYO.

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, katikati akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi nureyn yenye makao yake makuu mjini Iringa, Sheikh Saidi Abri (kulia) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango unaotolewa na Taasisi hiyo katika mjin wa Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla, kushoto mwenye suti nyeusi ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Alhaj, Majid Mwanga, hiyo ilikuwa wakati wauwekaji wa jiwe mawe ya msingi majengo mawili ya Wodi ya wazazi na jengo la wagonjwa wa dharula, majengo ambayo yamejengwa na Taasisi ya dhi Nureyn kwa kushirikiana na wahisani kutoka Saudi Arabia.

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,akimkabidhi cheti Mfadhili sheikh Saleh Bin Abdulazizi ambae ndiy aliyeleta fedha za kujengea majengo mawili ya wodi ya wazazi na jengo la wagonjwa mahututi ambayo yote yakiwa na thamani ya milioni mia tano, wanaoshuhudia kushoto ni mkuu wa Wilaya ya bagamoyo, Ahaj, Majid Mwanga na Mbunge wa jimbo la bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa.
 Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akihutubia wananchi katika viwanja vya hospitali ya Bagamoyo.
..........................................................

Serikali imesema inatambua mchango wa Taasisi ya kiislamu  ya Dhi Nureyn yenye makao yake makuu mjini Iringa katika kusadia shughuli za maendeleo.

Kauli hiyo imetolewa mjini Bagamoyo na Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alipokuwa akiweka mawe ya msingi kwenye majengo mawili katika Hospitali ya wilaya ya Bagamoyo.

Majengo hayo mawili yaliyowekwa mawe ya msingi ni jengo la wagonjwa wa dharula na jengo la wodi ya wazazi, ambayo yote hayo yamejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Dhi Nureyn wakishirikiana na wahisani kutoka Saudi Arabia.

Waziri Mwalimu alisema kitendo kilichofanywa na Dhi nureyn ni cha kizalendo na hivyo ndivyo wanavyotakiwa wawe watanzania wote katika kuisaidia serikali.
Alisema sera ya Afya ya mwaka 2007 inasema wadau wote wanawajibu wa kushirikiana na serikali katika kusadia upatikanji wa huduma bora za Afya.

Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi Nureyn, sheikh Saidi Abri  alisema malengo ya Taasisi hiyo ni kutoa huduma za kiroho, ki afya, ki elimu na kiuchumi, hivyo kufadhili majengo hayo yatakayosaidia katika huduma ya afya ni sehemu ya kazi yao.

Alisema mara baada ya kutembezwa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo wameguswa na hali waliyoikuta katika Hospitali hiyo na kuamua kusaidia ujenzi wa majengo hayo ili kuisaidia serikali katika shughuli za maendeleo.

Sheikh Abri alisema utoaji wa huduma bora za afya ni wajibu wa serikali lakini kila mtanzania anawajibika kuisaidia serikali katika kuhakikisha huduma bora za afya zinapatikana.

Alisema Taasisi ya Dhi nureyn kwa kuthamini sekta ya afya inasimamia uendeshaji wa zahanati 5 nne zikiwa vijijini na moja ikiwa jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa kutokana na umuhimu huo Taasisi hiyo kwa kushirikiana na mashirika ya nje ya nchi imeweza kuleta madaktari bingwa kutoka nchi mbalimbali kuja kutoa huduma ya matibabu ya macho katika mikoa ya nyanda za juu, kilimanjaro, Mbea na iringa.

Taasisi hiyo pia imeshawhi kuleta madaktari wa moyo kwa watoto ambapo mwaka 2016 Taasisi ya dhi nureyn imeleta Madaktari hao bingwa kwa magonjwa ya moyo katika hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na kufanikiwa kutibu watoto 188.

Akisoma Taarifa ya mradi wa ujenzi wa majengo hayo, Mganga mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Sylivia Mamkwe alisema kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia kuboresha huduma za afya katika Hospitali hiyo  na kuondoa msongamano uliopo sasa katika wodi ya wazazi.

alisema jengo la wazazi litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kulaza wazazi 30 kwa wakati mmoja huku kila mmoja akiwa kwenye chumba chake, na chumba cha kujifungulia kitakuwa na uwezo wa kulaza wazazi nane kwa wakati mmoja tofauti na sasa ambapo chumba cha kujifungulia kina uwezo wa kulaza wazazi watatu tu hali inayopelekea wazazi wengine kuzalishiwa wodini.

Mamkwe alisema ujenzi huo utagharimu jumla shilingi milioni 318 kwa jengo la wazazi na milioni 178 kwa jengo wagonjwa wa dharula.

Allisema Taasisi ya Dhi nureyn imeahidi kuweka vifaa tiba katika majengo hayo wanayojengwa ili huduma ziendelee kutolewa kama ilivyopangwa
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bagamoyo, Ally Ally alisema anamshukuru mkuu wa wilaya ya hiyo, Alhaji, Majid Mwanga kwa kufanikisha kupatikana kwa wafadhili hao ambao wameweza kujenga majengo ya thamani kubwa.

Alisema kutokana na juhudi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ni vyema jengo moja likaitwa Majid Mwanga ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka hata pale atakapoaandoka kwenye wilaya hiyo.

Ujenzi wa Majengo hayo yatakayoghrimu milioni mia tano yote mawili yameotokana na juhudi za mkuu wa Wilaya ya bagamoyo, alhaj, Majid Mwanga kuweza kuongea vizuri na wadau balimbali ambapo alifanikiwa kuzungumza na Taasisi ya Dhi nureyn yenye makao yake makuu mijini Iringa na kufanikisha ujenzi huo.

ujenzi huo pia ni muendelezo wa taasisi ya Dhi Nureyn katika kutoa huduma za jamii ambapo awali waliweza kuchimba visima katika mitaa ya Bagamoyo pamoja hospitali ya wilaya.

Jumla ya visima 38 vimechimbwa na Taasisi  Dhi nureyn katika Wilaya ya Bagamoyo, vikiwa na thamani ya shilingi milioni  mia sita kumi na nne, 614, ikiwa visima virefu kati ya hivyo ni 23 na vifupi ni 15.
 Diwani wa kata ya Kiromo wilayani Bagamoyo, Hassan R. Usinga, akipeana miokno na Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi nureyn yenye makao yake makuu mjini Iringa, Sheikh Saidi Abri.

Kata ya Kiromo ni miongoni mwa kata za wilaya ya Bagamoyo zilizofaidika na Miradi ya visima vya maji vilivyochimbwa na Taasisi ya Dhi Nureyn na kwamba kata ya Kiromo kupitia Diwani wake imeweza kutoa vyeti kwa wafadhili hao ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wao katika maendeleo ya jamii.
 Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akisikiliza Taarifa kutoka kwa Mganga mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Dkt. Sylivia mamkwe (hayupo pichani) kulia kwake ni mkuu wa wilaya ya bagamoyo, Alhaj, majid mwanga, wa kwanza kushoto ni Mfadhili wa miradi inayosimamiwa na Dhi nureyn Sheikh Saleh Bin Abdulazizi, na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Taasisi ya dhi nureyn, sheikh Saidi Abri.
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa anakagua majengo hayo mawili ya wodi ya wazazi na jengo la wagonjwa wa dharula yanayojengwa kwa ufadhili wa Dhi nureyn kwa kushirikiana na wahisani kutoka Saudi Arabia katika Hospitali ya wilaya Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment