Saturday, September 16, 2017

RTO PWANI APATA AJALI.



Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Pwani Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP. Abdi Isango amepata Ajali katika eneo la Kibiki, Msolwa Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Jonathan Shana amethibisha tukio hilo  na kusema kuwa Ajali hiyo imegusisha Gari Dogo aina ya Noah T.424 iliyokuwa likiendeshwa na Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani (RTO) na Roli lenye Namba za Usajili T.410 BEE.

Amesema Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo  Tarehe 16 mwezi huu wa Tisa 2017.

 Kamada Shana amesema katika Ajali hiyo mtu  mmoja amefariki ambae ni  baba mzazi  wa RTO huyo wa Pwani.
Na majeruhi wanne.

Kamanda Shana amemtaja Marehemu kuwa ni  Hamisi Isango ambae ni  baba mzazi wa Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Pwani na majeruhi ni Mkuu huyo wa Usalama barabarani Mkoa wa Pwani, Abdi Isango na mama yake  mzazi Zena Juma.

Wengine ni  wadogo zake Mkuu huyo wa Usalama barabarani Mkoa wa Pwani ambao ni  Haji Hamisi Isango na Shabani Hamisi Isango.

Majeruhi wote  wamelazwa katika hospitali  ya Tumbi kwaajili ya matibabu.

Kamanda Shana amesema chanzo cha Ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa roli ambae ameegesha Gari bila ya Tahadhari.

No comments:

Post a Comment