ZAHANATI KALIUA YATOA HUDUMA MASAA 24
ZAHANATI KALIUA YATOA HUDUMA MASAA 24 Na Allan Kitwe, Kaliua WAKAZI wa Kijiji Cha Zugimlole, Kata ya Zugimlole katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora wameeleza kufurahishwa na maboresho ya miundombinu ya Zahanati ya Kijiji hali iliyopelekea huduma kutolewa masaa 24. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa hali ya utoaji huduma katika Kata hiyo ilikuwa hafifu kutokana na kuchakaa miundombinu ya Zahanati hiyo kongwe, hali iliyopelekea akinamama kujifungulia nyumbani kwao. Mariamu Nzumbe (50) mjasiriamali mkazi wa Kijiji hicho amepongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha huduma katika zahanati hiyo ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu akinamama kufuata huduma hizo katika Vijiji vingine. ‘Kwa sasa tunapata huduma zote hapa hapa tofauti na huko nyuma, hata w...