Posts

ZAHANATI KALIUA YATOA HUDUMA MASAA 24

Image
  ZAHANATI KALIUA YATOA HUDUMA MASAA 24 Na Allan Kitwe, Kaliua                                                       WAKAZI wa Kijiji Cha Zugimlole, Kata ya Zugimlole katika Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Mkoani Tabora wameeleza kufurahishwa na maboresho ya miundombinu ya Zahanati ya Kijiji hali iliyopelekea huduma kutolewa masaa 24. Wakizungumza kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa hali ya utoaji huduma katika Kata hiyo ilikuwa hafifu kutokana na kuchakaa miundombinu ya Zahanati hiyo kongwe, hali iliyopelekea akinamama kujifungulia nyumbani kwao. Mariamu Nzumbe (50) mjasiriamali mkazi wa Kijiji hicho amepongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuboresha huduma katika zahanati hiyo ili kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu akinamama kufuata huduma hizo katika Vijiji vingine. ‘Kwa sasa tunapata huduma zote hapa hapa tofauti na huko nyuma, hata w...

SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA

Image
  SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA Na Allan Kitwe, Tabora JUMLA ya silaha za moto 17 na risasi 19 zimesalimishwa kwa hiari katika Vituo vya Polisi na Ofisi za Serikali za Vijiji na Kata Mkoani Tabora kufuatia zoezi linaloendelea nchi nzima la usalimishaji silaha haramu kwa hiari bila kushtakiwa. Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Lulengelule, alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa zoezi hilo limeanza Septemba 1, 2026 na litamalizika Oktoba 31, 2026. Amefafanua kuwa zoezi hilo linaloendeshwa na Jeshi la Polisi nchi nzima limelenga kuhakikisha silaha haramu zote zikiwemo zile zinazomilikiwa na watu au taasisi kinyume na taratibu zinasalimishwa kwa hiari kwa msamaha pasipo kushtakiwa. ‘Zoezi hili ni muhimu sana, naendelea kutoa wito kwa wananchi kutekeleza kwa hiari kabla ya kipindi cha msamaha wa kutokushtakiwa kumalizika ifikapo Oktoba 31, 2026 kinyume na hapo mkondo wa sheria utachukua...

TAKUKURU KAGERA YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 2.

Image
  Na Alodia Babara,  Bukoba. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera imefanikisha uokoaji wa zaidi ya sh bilioni 2.7 kutoka kwa makampuni binafsi 146 yaliyokuwa wadaiwa sugu wa michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kati ya jumla ya Sh5.2 bilioni zilizokuwa zinadaiwa. Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kagera Ismail Bukuku akizungumza na waandiahi wa habari Septemba 16, 2026 amesema, hatua hiyo imechukuliwa baada ya ofisi yake kufuatilia madeni hayo na kuchukua hatua dhidi ya waajiri waliokuwa hawawasilishi kwa wakati fedha za michango ya wafanyakazi wao katika mfuko huo. "Waajiri hawa walishindwa kulipa michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miaka 9 kuanzia mwaka 2017 hadi Julai 2026 iliyofikia kiasi cha sh bilioni 5.2" amesema Bukuku Alieleza kuwa, oparasheni hiyo ilifanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza oparasheni ilianza Julai 22 hadi Agosti 5 huku awamu ya pili ...

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 16 SEPTEMBA 2026

Image
 

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 13 SEPTEMBA 2026

Image
 

MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 12 SEPTEMBA 2026

Image