MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AZITAKA WIZARA ZENYE DHAMANA YA ELIMU KUFANYIA KAZI TAFITI ZILZOFANYIKA KUHUSU LUGHA IPI INAFAA KUFUNDISHIA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizindua Kamusi Maalum kwaajili ya Shule za Msingi Pamoja na mkakati wa Taifa wa kubidhaisha ndani na nje ya nchi kwa mwaka 2022-2032 wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani iliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 7 Julai 2022. ........................................... Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amezitaka Wizara zenye dhamana ya Elimu kufanyia kazi matokeo ya tafiti nyingi ambazo zimefanyika kuhusu lugha ipi inafaa kufundishia ili Serikali ifanye uamuzi na hatimaye watoto na vijana wa Kitanzania waanze kujifunza kwa lugha yao ya kiswahili kuanzia shule ya awali hadi Chuo Kikuu. Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. ...