Popular posts from this blog
MAGAZETI YA LEO TAREHE 19 SEPTEMBA 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAGAZETI YA TANZANIA LEO TAREHE 13 SEPTEMBA 2026
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
DC SHAKA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA KODI KILOSA Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Shaka Hamdu Shaka, leo ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Kodi ya Wilaya kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Kikao hicho kimejadili tathmini ya mwenendo wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2025/2026 na kuweka mikakati ya kuimarisha makusanyo kwa mwaka 2026/2027. Akizungumza katika kikao hicho, Shaka amesema kazi ya kukusanya kodi sio ukusanyaji tu, bali ni ujenzi wa maendeleo. "Sisi sio wakusanya kodi tu, bali ni wajenzi wa maendeleo. Kila shilingi tunayokusanya kwa haki na uadilifu, tunajenga kesho bora ya wananchi wetu. Hivyo jukumu letu sio dogo," alisema Shaka. Aidha, Shaka ameelekeza kila chanzo cha mapato Wilayani humo kipitiwe upya. "Kile ambacho kimekufa kifufuliwe, kile ambacho kinalala kiamshwe. Lazima tubadili mtazamo kutoka kudhibiti kwenda kuelimisha umma," alisisitiza. Ameitaka TRA na Halmashauri kuimarisha matumizi ya takwimu halisi (Da...
MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS AAGIZA HATUA ZA HARAKA KUJIANDAA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MVUA ZA EL NIÑO Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagiza Mamlaka na Taasisi zinazohusika kuchukua hatua za haraka kujiandaa ili kuzuia na kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño zinazotarajiwa kuanza mwezi Oktoba 2026. Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo, mara baada ya kupokea taarifa ya utayari na maandalizi ya Serikali kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuhusu mvua za El- nino, katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Viongozi pamoja na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zilizochini ya Wizara hizo, Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa taasisi zote zinazohusika, kufanya kazi kwa pamoja na kuchukua hatua za tahadhari mapema ili kuzuia au ku...
MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS AMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, UTOAJI WA TUZO ZA PYMA. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji wa tuzo za 19 za Rais za Wazalishaji Bora Viwandani, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na wazalishaji wa saruji nchini, kuhakikisha wanatafuta suluhu ya haraka ili kurejesha bei ya kawaida ya saruji kwa wananchi. Amesema maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanaweza kununua mfuko wa saruji kwa gharama nafuu hivyo ni lazima kuoanisha uzalishaji wa malighafi zote zinazochangia katika uzalishaji wa saruji ili bidhaa hiyo ipatikane kwa urahisi. Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema ni muhimu kufanya tathimini ya ukuaji wa viwanda hapa ...
SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
SILAHA 17 ZA MOTO ZASALIMISHWA TABORA Na Allan Kitwe, Tabora JUMLA ya silaha za moto 17 na risasi 19 zimesalimishwa kwa hiari katika Vituo vya Polisi na Ofisi za Serikali za Vijiji na Kata Mkoani Tabora kufuatia zoezi linaloendelea nchi nzima la usalimishaji silaha haramu kwa hiari bila kushtakiwa. Hayo yamebainishwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Twaha Lulengelule, alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa zoezi hilo limeanza Septemba 1, 2026 na litamalizika Oktoba 31, 2026. Amefafanua kuwa zoezi hilo linaloendeshwa na Jeshi la Polisi nchi nzima limelenga kuhakikisha silaha haramu zote zikiwemo zile zinazomilikiwa na watu au taasisi kinyume na taratibu zinasalimishwa kwa hiari kwa msamaha pasipo kushtakiwa. ‘Zoezi hili ni muhimu sana, naendelea kutoa wito kwa wananchi kutekeleza kwa hiari kabla ya kipindi cha msamaha wa kutokushtakiwa kumalizika ifikapo Oktoba 31, 2026 kinyume na hapo mkondo wa sheria utachukua...
NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS MHE. NDEJEMBI AAGIZA DAMPO LA PUGU LIBORESHWE, KERO ZA WANANCHI ZITATULIWE Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Halmashauri zake kuhakikisha hali ya Dampo la Pugu inaboreshwa, huku akielekeza maeneo ya makazi yanayozunguka dampo hilo kupuliziwa dawa ili kuwalinda wananchi dhidi ya wadudu na kupunguza hatari ya magonjwa, hususan katika kipindi cha mvua. Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 18, 2026, alipofanya ziara katika Dampo la Pugu linalotumika kukusanya taka za Mkoa wa Dar es Salaam ili kujionea hali halisi ya eneo hilo na kusikiliza kero za wananchi wanaoishi maeneo ya jirani. Aidha, ameelekeza kuandaliwa kwa mpango kazi wa pamoja utakaoainisha hatua za haraka na za muda mrefu za kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa Dampo la Pugu pamoja na kero zinazowakabili wananchi wanaoishi katika maeneo yanayolizunguka, ikiwemo kutopuliziwa dawa ...
SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
SHAIBU NDEMANGA, ACHANGIA CEMENT 50 SHULE YA SIRAJULMUNIR BAGAMOYO. Na Athumani Shomari Bagamoyo. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga amechangia mifuko 50 ya Cement kwaajili ya ujenzi wa bwalo la chakula katika shule ya Msingi Sirajulmunir iliyopo kata ya Nianjema wilayni Bagamoyo. Mkuu huyo wa wilaya ametoa Ahadi hiyo hivi karibuni, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 16 ya wahitimu wa darasa la saba, katika shule hiyo. Akizungumza kwa niaba yake, Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya, Ibrahim Gama amesema juhudi zinazo oneshwa na shule hiyo zinapaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo ndani na nje ya Bagamoyo. Amesema Watoto wanaosoma Shule ya Sirajulmunir wana uwezo mkubwa katika masomo hali inayopelekea kila mwaka kufanya vizuri katika mitihani yao ya kuhitimu elimu ya msingi na wanakuwa Watoto wenye maadili mema katika jamii. Aliongeza kwa kusema kuwa, ufasaha wa lugha ya kingereza, kiarabu, ufaulu mzuri na maadili mema ni Ishara kubwa ya ubora wa elimu inayotolewa s...
MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI.
By
BAGAMOYO KWANZA BLOG
-
MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini yake katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Jumatano Septemba 09, 2026. Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo. Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa Viongozi na Watendaji hao kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Wasaidizi wake ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia Watanzania. Aidha, Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa...




























Comments
Post a Comment