Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo Bwana Shauri Selenda leo tarehe 23 Oktoba 2023 ameiagiza Kamati ya Lishe Halmashauri ya Bagamoyo kusimamia na kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na bustani ya mbogamboga pamoja na matunda Ili kujenga afya Kwa wanafunzi na jamii Kwa ujumla.
Akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe na kupokea taarifa ya utendaji kazi wa Kamati hiyo Selenda alisisitiza kuwa, Kwa Sasa suala la Lishe lazima kupewa kipaumbele kwani jamii yetu kwa sasa inashindwa kulitilia uzito.
" Niseme tuu kuwa tuwasaidie wananchi wetu katika masuala ya Lishe ni jukumu letu na tuhakikishe kuwa kila shule inakuwa na eneo kwaajili ya bustani ya mboga na matunda hakikisheni mntekeleza hilo na nitapita kila shule kufanya ufuatiliaji wa suala hili". Alisema Bwana Selenda.
Kamati ya Lishe Halmashauri ya Wilaya Bagamoyo imekutana kujadili taarifa mbalimbali za masuala ya Lishe robo ya kwanza Mwaka wa fedha 2023/2024.
No comments:
Post a Comment