RAIS SAMIA AMPOKEA RAIS WA BURUNDI NDAYISHIMIYE KUANZA ZIARA YA SIKU 3 NCHINI

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye  mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba, 2021 kwa ziara ya kikazi ya siku 3.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakati nyimbo za Mataifa mawili Tanzania na Burundi pamoja na wimbo wa Afrika Mashariki  zikipigwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na  Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtambulisha mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwa Viongozi mbalimbali wa Serikali mara kuwasili katika viwanja vya Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 22 Oktoba 2021.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo Rasmi na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye aliyekuwa akiongoza ujumbe kutoka Burundi katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari wakati wa ujio wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

No description available.

Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evareste Ndayishimiye akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

PICHA NA IKULU.

 

Comments

Popular posts from this blog

VEDMA KUCHONGA BARABARA KIMANGE - PONGWE MNAZI

MATOKEA DARASA LA SABA 2018 HAYA HAPA.

RAIS WA ZANZIBAR ATOA POLE KUFUATIA KIFO CHA MAMA FATMA KARUME.

MWANRI AWAPA SOMO MAKADA WALIONOLEWA.

TITF YAANDAA TAMASHA LA SANAA ZA UFUNDI ARUSHA

MADIWANI CHALINZE WAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.

WAZEE WAASWA KUWA MBELE KATIKA KUHAMASISHA USHIRIKI WA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

VIJANA MANISPAA TABORA WALAMBA MKOPO WA MIL 109