Halmashauri ya Bagamoyo wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imepokea Bilioni 1.4 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo.
Fedha hizo ni sehemu ya fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwa Tanzania, ambazo ni shilingi Trilioni 1.3 kwaajili ya Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.
Wakati huohuo Halmashauri ya Chalinze imepokea jumla ya shilingi milioni 250 ikiwa ni mgao wa tozo za serikali zinazotokana na miamala ya simu ambazo zitatumika kujenga kituo cha Afya Fukayosi.
Eneo ambalo litajengwa kituo cha Afya Fukayosi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Ndg.Shauri Selenda akikagua eneo ambalo litajengwa kituo cha Afya Fukayosi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo Ndg.Shauri Selenda akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Udindivu kata ya Mapinga.
No comments:
Post a Comment