Friday, October 22, 2021

TAKUKURU KUTUMIA SKAUTI KUPAMBANA NA RUSHWA.

 No description available.

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tabora Mussa Chaulo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo Pichani).

...................................................

Na Lucas Raphael,Tabora

    

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU- Mkoa wa Tabora Imejipanga kuhakikisha inadhibiti mianya ya Rushwa katika fedha zilizotolewa na Serikali kwenye Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wakiwemo Skauti.

 

Akitoa taarifa ya utendaji kazi ya Miezi Mitatu iliyopita Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tabora Mussa Chaulo Alisema kuwa chama cha Skauti Tanzania ni moja ya Wadau wakubwa ambao wakishirikiana nao kwa ukaribu mianya mingi ya Rushwa Itazibika.

 

Mkuu huyo wa Takukuru amesema kuwa lengo la kushirikisha wadau wengi ni kudhibiti fedha ambazo zimetolewa na Serikali kuboreshea huduma katika sekta za Elimu na Afya zifanye kazi iliyokusudiwa.

 

Chaulo alisema Takukuru Mkoa wa Tabora imejipanga Kuzuia na kupambana na rushwa msisitizo ukiwekwa kwenye ufuatiliaji wa fedha zilizopelekwa na Serikali ndani ya Halmashauri kwa ajili ya Miradi mbali mbali.

 

Alisema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita wameweza kufuatilia Miradi ya Maendeleo 13 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 4.7.

 

Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Tabora Mjini, Maabara katika shule za sekondari  Inala,Umiki na Ugala, ujenzi wa vyuo vya Veta Wilaya za Uyui na Igunga pamoja na Barabara ya Lami ya Igumba hadi Mbiti.

 

Chaulo alisema kuwa mapungufu yaliyopatika na ambayo yangeweza kusababisha miradi husika kutokamilika kwa kiwango stahili yalifanyiwa kazi kwa kuweka vikao na wadau husika kwa lengo la kuondoa mianya ya Rushwa na kusisitiza uzingatiaji wa Sheria na kanuni za Manunuzi.

 

Katika hatua nyingine Takukuru mkoa wa Tabora ilipoeka jumla ya malalamiko 68, ambapo 45 yalikuwa na viashiria vya Rushwa  na 23 hayakuwa na viashiria vya rushwa.

 

Mkuu huyo wa Takukuru alisema kuwa malalamiko hayo yalifunguliwa majalada ya Uchunguzi ambapo sita uchunguzi wake umekamilika, 33 uchunguzi bado unaendelea huku mengine sita majalada yakiwa yamefungwa kutokana nakukosekana kwa ushahidi.

 

Halikadhalika kulikuwa na Miradi mitatu iliyokataliwa kuwekewa mawe ya msingi na Kiongozi wa mbio Maalumu za Mwenge wa Uhuru mwaka huu wa 2021 uchunguzi wake bado unaendelea kufanyiwa kazi.

No comments:

Post a Comment