Friday, October 22, 2021

MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA TANO WA TEHAMA

 No description available.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kwa Tuzo kutoka kwa Waziri wa  Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji  kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kukuza sekta ya TEHAMA Nchini.  katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Tehama Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.

No description available.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha nakala za mwongozo wa usajili wa  watalaamu wa Tehama baada ya kuuzindua,  katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Tehama Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021. Kushoto ni Waziri wa  Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji.

 No description available.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa Sekta ya TEHAMA wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha.

No description available.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza, Mkurugenzi wa Masuala ya Sekta kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Emmanuel Manasseh  (kushoto) wakati alipotembelea banda la TCRA katika Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021.  Wa pili kushoto ni Waziri wa  Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella.

No description available.

Wadau wa Sekta ya TEHAMA wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa TEHAMA Tanzania uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) jijini Arusha, Oktoba 22, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment