Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Mhandis Abnery Mganga, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
...................................................................
NA HADIJA OMARY- LINDI.
TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Lindi imeanzisha mpango wa Takukuru inayotembea itakayowawezesha kufahamu na kufanyia kazi kero mbali mbali za wananchi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Taasisi hiyo, kwa kipindi cha julay hadi Septemba 2021, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Mhandis Abnery Mganga, amesema kuwa, kwa kutekeleza Mpango huo maafisa wa Takukuru huambatana na wakuu wa Idara za halmashauri ili kuweza kutatua kero za wananchi .
Alieleza kuwa katika Mpango huo wananchi wengi wamejitokeza na kulalamikia Matumizi mabaya ya Madaraka ya viongozi katika maeneo ya kata na vijiji ikiwemo kutopewa taarifa juu ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao pamoja na kutosomwa mapato na matumizi ya miradi inayosimamiwa na ngazi ya vijiji na kata.
Aidha alitaja migogoro ya Aridhi isiyoisha, tozo Mbali mbali za Halmashauri, kuchelewa kupata malipo ya mazao yao baada ya kuuzwa na ubadhirifu wa viongozi ni miongoni mwa kero kubwa walizozigundua katika ufuatiliaji huo.
Hata hivyo Mganga ameeleza kuwa katika kipindi hiko jumala ya malalamiko shauri 81 yalipokelewa , kati ya hayo 48 yalihusu Rushwa na 33 hayakuhusu Rushwa ambapo alisema kuwa kati ya malalamiko hayo 48 yanayohusu rushwa yalifunguliwa majalada ya uchunguzi ambapo majarada 46 yanaendelea na majalada 2 yamekamilika huku taarifa 33 ambazo hazihusu Rushwa zikihamishiwa katika idara nyingine kwa hatua zaidi.
Mganga pia ameeleza namna Taasisi hiyo ilivyojipanga katika kuendelea na kufuatilia miradi mbali mbali ya kimkakati kwenye Mkoa huo katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwemo ya ujenzi wa Barabara vijijini, ujenzi wa Madarasa, Zahanati pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Maji tandangongoro .
No comments:
Post a Comment