Wednesday, October 27, 2021

RAIS SAMIA ATAKA USHIRIKIANO TAMASHA LA BAGAMOYO.

 No description available.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya  Wanawake Twiga Stars mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Cosafa kwa Timu  hiyo leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

..............................................

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka watendaji katika wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na wadau mbalimbali wa Sanaa, Utamaduni na Michezo kushirikiana kufanikisha Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni litakaloanza kesho Tarehe 28 Oktoba 2021 katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, (TaSUBa).

 

Rais Samia ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Viongozi na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya  Wanawake Twiga Stars mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Cosafa kwa Timu  hiyo leo tarehe 27 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

Alisema hivi karibuni limefanyika Tamasha la kwanza la michezo kwa wanawake ambalo limefanyika mafanikio makubwa.

 

Mh. Rais Samia amepongeza sana juhudi zinazofanyika katika kukuza Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuunga mkono juhudi na muelekeo wa serikali.

 

Aidha, amekumbusha hutuba yake aliyoitoa Sept. 08. 2021 wakati alipokabidhiwa rasmi uchifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Chifu Hangaya huko Mkoani Mwanza, ambapo alipendekeza Tamasha la kitaifa la utamaduni litakalofanyika kila mwaka katika kila mkoa ambapo mikoa hiyo ishindanishwe ili kumpata mshindi.

 

Alisema ametoa wazo hilo la Tamasha la kitaifa la utamaduni lengo ni kukuza utamaduni wa mtanzania.

 

Tamasha la 40 la kimataifa la Sanaa na Utamaduni litazinduliwa kesho Tarehe 28 Oktoba na kufungwa Tarehe 30 Oktoba 2021 katika viwanja vya TaSUBa ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya sanaa na utamaduni kutoka vikundi vya ndani nje ya nchi.

 

Zaidi ya vikundi 60 vya ndani ya Tanzania vimethibitisha kushiriki huku nchi zaidi ya tano zimethibisha kushiriki katika Tamasha hilo la Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment