Tuesday, October 19, 2021

DC TEMEKE AIPONGEZA SHULE YA YEMEN DYCCC.

 No description available.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo amepongeza uongozi wa shule za Yemen DYCCC kwakusimamia utoaji wa elimu bora katika shule zake na kuipa sifa wilaya hiyo.

Katika hutuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Afisa Elimu Msingi, Rashid Ally, amesema elimu bora ndio inayomjenga mtoto katika maisha yake ya baadae, kwa familia yake, jamii inayomzunguuka na Taifa kwa ujumla.

Rashid alisema anamuwakilisha Mkuu wa wilaya ya Temeke na kwamba salamu za Mkuu wa wilaya hiyo ni kuupongeza uongozi wa Yemen DYCCC kutokana na kusimamia utoaji wa elimu bora katika shule zake.

Alisema kitendo cha kutoa elimu ni kuunga mkono juhudi za serikali, hivyo uongozi wa wilaya utakuwa pamoja na uongozi wa Yemen DYCCC katika kuhakikisha shule hiyo inaendelea kutoa elimu bora.

Aidha, katika kuhakikisha elimu bora inapatikana shuleni hapo amewataka wazazi kulipa ada kwa wakati ili kuiwezesha shule kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika kufundisha watoto.

Nae Mwenyekiti wa Bodi ya Elimu ya DYCCC, Hassan Akrabi amesema kazi kubwa waliyonayo ni kuhakikisha mtoto anakuwa na maadili mema katika kipindi chote anapokuwa shuleni ambapo hali hiyo itamjenga kuishi katika maadili mema pia hata akiwa nje ya shule.

Aidha, aliwataka wahitimu hao kuendeleza maadili mema waliyoyapata wakiwa shuleni hapo ili waweze kuendelea kutafuta elimu huku wakiwa na maadili mema.

Aliwataka wazazi kuendelea kuwaamini na kuwaomba watoto wanaoanza kidato cha kwanza wapelekwe katika shule ya Sekondari ya Yemen DYCCC ili wakaendelezwe katika malezi yenye maadili.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Yemen DYCCC, Rahim Burhan, alisema shule hiyo imepata mafanikio mbalimbali toka kuanzishwa kwake mwaka 2003 ambapo kwa sasa shule inamiliki jengo la kisasa la ghorofa tatu ambalo linajumuisha madarasa 36, ofisi 18, vyoo 52, stoo 02, maktaba 01, chumba cha maabara 01, maabara ya Computer 01, na ukumbi ambao hutumika kwaajili ya ibada ya swala.

 No description available. 

Kaimu Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Temeke, Rashid Ally, akizungumza katika mahafali ya Darasa la saba 2021 katika shule ya Msingi Yemen DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam.


No description available.No description available.

Wahitimu wa darasa la saba, Shule ya Msingi Yemen DYCCC iliyopo Chang'ombe jijini Dar es salaam wakifuatilia kwa umakini kinchaoendelea katika mahafali yao yaliyofanyika shuleni hapo.


No description available.

  

No comments:

Post a Comment