Mkuu
wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah (katikati) akizungumza na waandishi wahabari (hawapo pichani) kuhusu Tamashala la 40 Kimataifa la Sanaa na Utamaduni litakalofunguliwa rasmi siku ya Alhamisi tarehe 28 oktoba 2021, wa tatu kushoto ni
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Dkt. Herbert
Francis Makoye.
...................................................................
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah, amewakaribisha wananchi ndani na nje ya Bagamoyo kuhudhuria Tamasha la 40 la kimataifa la sanaa na Utamaduni litakalofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) siku ya tarehe 28 Oktoba 2021 hadi 30 Oktoba 2021.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika ukumbi wa TaSUBa, Mkuu huyo wa wilaya ya Bagamoyo amesema Tamasha hilo la kimataifa la sanaa na utamaduni ni fursa ya kipekee kwa wasanii kuonyesha kazi zao mbele ya wageni watakaohudhuria hilo.
Alisema katika Tamasha hilo zipo fursa nyingi kwa wasanii, wananchi wa kawaida pamoja na serikali kwa ujumla.
Akifafanua zaidi DC. Zainab alisema kwa wasanii ni fursa ya kuonyesha kazi zao kwa waliohudhuria wakiwemo wageni kutoka nje ya nchi na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa sanaa na utamaduni.
Aidha alisema wananchi wanaweza kutumia fursa hiyo ya Tamasha kujifunza namna sanaa inayoweza kumuinua kijana wa kitanzania na kumfanya sio tu mtoa burudani kwa jamii lakini pia ikampatia kipato kwaajili ya kuendesha maisha yake.
Aliongeza kwa kusema kuwa, Serikali pia itatumia fursa hiyo ya Tamasha la sanaa kutangaza vivutio vilivyopo Bagamoyo ambapo wageni watweza kujionea maeneo mbalimbali ya kihistoria yaliyopo ndani ya Bagamoyo na hivyo watakapoweza kutembelea vivutio hivyo serikali itaingiza mapato kupitia watalii hao.
Alisema kutokana na umuhimu wa Tamasha hilo kwa wageni kutoka nje ya Bagamoyo na nje ya Tanzania kutakuwa na punguzo maalum la bei katika hoteli zote za Bagamoyo ili kuwarahisishia wageni kupata sehemu za kulala kwa gharama nafuu.
Mkuu huyo wa
wilaya amesema kutokana na mapambano dhidi ya ugonjwa Corona, kama wilaya
itatumika nafasi hiyo kuweka banda maalum lakupata chanjo ya uviko19, kwa wale
ambao bado hawajapa chanjo hiyo ili iwe rahisi kwao kuchanja huku wakiendelea na burudani kwa siku zote tatu za Tamasha hilo.
Wakati huohuo, Mkuu huyo wa wilaya ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, amewahakikishia wageni wote wilayani humo kuwa, wilaya ya Bagamoyo ipo salama na kwamba wataweza kutembea maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo bila ya bghudha ya aina yoyote.
Alisema wilaya ya Bagamoyo ni tulivu na haina vitendo vyovyote vya uhalifu na kwamba ulinzi utaimarishwa zaidi siku za Tamasha.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Dkt. Herbert Francis Makoye, alisema wanajinia kuendelea kuandaa matamasha kila mwaka ndani ya chuo hicho tamasha la mwaka huu ni la 40.
Alisema yapo matamasha mengi yanaanzishwa hapa nchini lakini hayana muendelezo kwa TaSUBa kuendelea kuandaa Tamasha kila mwaka ni mafanikio makubwa ya kujivunia ndani ya chuo, kwa viongozi wa wilaya, wizara na Taifa kwa ujumla.
Dkt. Makoye alisema Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo hufanyika kila mwaka na huandaliwa na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) chini ya Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo likiwa na malengo ya
· Kutunza na kuenzi sanaa na utamaduni wa mtanzania.
· Kutengeneza jukwaa ambalo wanafunzi wa TaSUBa wanalitumia kupima viwango vyao vya umahiri katika sanaa kwa mwaka katikia fani za sanaa za maonyesho na zile za ufundi.
· Kukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za dunia ili kuonyesha utajiri wao wa sanaa na utamaduni.
· Kutenegeneza jukwaa ambalo ni kiungo cha kujenga mahusiano ya wasanii wa ndani na nje ya nchi kupitia maonyesho ya sanaa.
· Kubadilishana uzoefu na mawazo katika kuendeleza tasnia ya sanaa.
· Kutoa burudani kwa watanzania na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Tamasha la mwaka huu litapambwa na ngoma za asili, muziki wa kizazi kipya, singeli, sarakasi, mazingaombwe, maigizo pamoja na maonyesho na biashara ya sanaa na ufund.
Aidha, Dkt. Makoye aliongeza kuwa, katika Tamasha hilo kutakuwa na warsha na semina zitakazohusu mambo mbalimbali katika Nyanja za sanaa na utamaduni.
Alisema jumla ya vikundi ambavyo vimethibitisha kushiriki ni 70 ambapo vikundi vya ndani ya nchi ni 60 na vikundi 10 kutoka nje ya nchi.
Tamasha litafunguliwa rasmi siku ya Alhamisi Tarehe 28 Oktoba 2021 likitanguliwa na mkesha siku ya Jumatano tarehe 27 Oktoba 2021 ambapo kila siku kutakuwa na mgeni mashuhuri na litafungwa rasmi siku ya jumamosi tarehe 30 Oktoba 2021.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Dkt. Herbert Francis Makoye, (aliyesimama) akizungumza wakati wa kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Bi Zainab Abdallaah (wa tatu kulia).
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Abdallaah (wa nne kushoto) amkiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakufunzi na wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment