Thursday, October 21, 2021

RAIS SAMIA MGENI RASMI UWT PWANI.

 No description available.

Na Mwamvua Mwinyi, PWANI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika, mkutano wa kilele Cha wiki ya UWT Taifa na kumuenzi muasisi na mwanamke Shupavu Bibi Titi Mohammed oktoba 23 mwaka huu, huko Ikwiriri Rufiji, viwanja vya Ujamaa.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Pwani, Mwenyekiti wa UWT Taifa ,Gaudensia Kabaka amesema ,pia wanatarajia kutembelea wagonjwa na  kutoa vitu mbalimbali katika vituo vya afya na wanafunzi wa shule ya wasichana Ikwiriri.

 

“Tumeona Mgeni rasmi awe Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ,mwana UWT mwenzetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,”Tumeamua kuadhimisha kilele hicho Rufiji kwa sababu ya historia ya mama na mwanamke shupavu aliyemsaidia Baba wa Taifa Mwl.Nyerere kupigania Uhuru Bibi Titi Mohammed.

 

“Wiki ya UWT ilivyoanza ilianzishwa na chama Cha TANU ilikuwa sehemu ya wanawake wa TANU na Mwl.Nyerere alikuwa akisaidiwa na Bibi Titi, ambae alikuwa mhamasishaji mzuri ,muasisi na alikuwa Shupavu “

 

“Mwaka 1977 chama Cha TANU na ASP, umoja ikaanzishwa UWT na mwenyekiti wake akaendelea kuwa Bibi Titi.”

Akielezea wiki hiyo,Kabaka alifafanua maadhimisho hayo yameanza Tarehe 27 septemba hadi Tarehe 04 oktoba kwa kujitangaza na kufanya shughuli mbalimbali ,ambapo kauli mbiu Ni “TUNAHUSISHA KUMKOMBOA MWANAMKE KIUCHUMI ,KIFIKRA NA KISIASA.

 

Alisema mwanamke anapaswa kujikomboa kiuchumi kwa kujishughulisha kusaidiana na baba sambamba na wazazi watambue kuwasomesha watoto wote bila kuwabagua.

 

Hata hivyo Kabaka, aliomba wanawake wajitokeze Rufiji kuadhimisha shughuli hiyo na kumuenzi Bibi Titi Mohammed na kuungana na Rais Samia ambae atakuwa mgeni rasmi.

 

Kuhusu Rais Samia Sina haja ya kueleza ushupavu wake maana ameweza pia kutupatia trilioni 1.3 kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kupambana na ugonjwa wa Uviko19 pamoja na ujenzi wa madarasa na vituo vya afya.

 

Nae Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alisema licha kuhakikisha sherehe hizo zinafanyika Pwani lakini kumuenzi Bibi Titi Mohammed kwa ukombozi wake.

Alisema hii itasaidia kuutangaza mkoa , kujua historia na kuutangaza kiutalii.

 

Kunenge alieleza, ni dhahiri Rais  Samia anapita katika nyayo za Bibi Titi kwa kuwa Shupavu ambapo katika mkoa wa Pwani ipo miradi ya maji iliyopatiwa fedha kupitia DAWASA ,mradi mkubwa wa bwawa la umeme Stigo-Rufiji tilioni 2.8 zimeshalipwa ,mradi wa Daraja jipya WAMI bilioni 72,Mradi wa reli ya kisasa (SGR) unaogharimu bilioni 37 hivyo wanaPwani wana kila sababu ya kumpenda Rais Samia kwa miradi mikubwa na ya kati inayoendelea .

No description available.

 

No comments:

Post a Comment