Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira
Mgalu akizungumza jambo kuhusiana na mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya
kuweka mipango ya kuunganisha nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda
vipya 50 wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini
ambayo ilifanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo
katika Wilaya ya Mkuaranga. (Picha na Victor Masangu).
.....................................
VICTOR
MASANGU, MKURANGA.
Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu
amesema katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025 serikali imedhamiria kusambaza na kuwaunganishia nishati ya umeme wa
gesi asilia katika viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vimepitiwa na
bomba la gesi ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam Pwani pamoja na Mtwarana.
Mgalu aliyasema hayo wakati wa
ziara ya kikazi ya kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini ambayo wameifanya
kwa lengo la kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo Wilayani Mkuranga Mkoa wa
Pwani ambavyo vinajiendesha kwa kutumia nishati ya umeme ikiwa ni pamoja
na kuzungumza na wawekezaji ili kubaini changamoto wanazokabiliana nazo na
kuzitafutia ufumbuzi.
Naibu Waziri huyo alibainisha kwamba
kwa sasa serikali ya awamu ya tano mpango wake mkubwa ni kuhakikisha inasambaza
na kuviunganishia viwanda mbali mbali nishati ya umeme ili viweze kutimiza
malengo ya azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kutoa fursa
mbali mbali za ajira kwa vijana ambao ni wazalendo lengo
ikiwa waweze kujikwamua na wimbi la umasikini.
“Mpango wetu wa serikali licha ya kuwa
bado kuna baadhi ya maeneo ya viwanda hayajafikiwa na nishati ya umeme lakini
kwa sasa kupitia nishati ya gesi asilia tuna mpango wa kuviunganishia viwanda
vipya vipatavyo 50 ambavyo vipo katika Mikio ya Dar es Salaam, Mtwara pamoja na
Mkoa wa Pwani hivyo juhudi za makusudi bado zinaendelea kwa hiyo viwanda
ambavyo vinapitiwa na bomba kubwa la gesi vitaweza kunufaika.
Aidha Naibu Waziri huyo alifafanya
kwamba pindi mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere uliopo Wilayani Rufiji
utakapokamilika utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wawekezaji wa viwanda
vidogo, vya kati na vile vikubwa kutoka maeneo mbali mbali sambamba na
kuwaunganishia wananchi wengine pamoja na taasisi za serikali na sizozo
za serikali.
Katika hatua nyingine Mgalu ameipongeza
kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini kwa kuweza kwenda kutembelea
katika kiwanda cha kuzalisha chuma pamoja na mabomba ya maji ili kuweza kubaini
changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wawekezaji na hatimaye kuweza
kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambao utasaidia kutimiza azma ya serikali ya
kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda hivyo.
Kwa upande wake Kaimu mwenyekiti
wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini Vedastus Matayo alibainisha
kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaweza kuipunguzia serikali gharama kubwa
ambazo zimekuwa zikitumia kwa ajili ya kuagiza baadhi ya Nondo kutoka nje ya
nchi hivyo amempongeza mwekezaji huyo kwa kuwekeza katika Wilaya ya
Mkuranga kwani kumesaidia vijana zaidi ya 1,300 kupata fursa ya ajira.
“Sisi kama kamati kwa kweli tunapenda
kumpongeza mwekezaji huyo kwa kuweza kuwekeza katika Wilaya ya Mkuranga ambayo
ipo katika Taifa letu ya Tanzania hii ni hatua nzuri ambayo ameifanya na kwa
sasa anazalisha bidhaa mbali mbali kwa kutumia nishati ya umeme wa gesi asilia
hivyo kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wenyewe
pamoja na wale wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,”alibainisha Matayo.
Aidha Matayo katika hatua nyingine
alibainisha kuwa Kamati ya bunge ya nishati ya kudumu ya nishati na
madini ilibaini kuwepo kwa urasimu na ucheleweshaji wa vibali
kutoka kwa baaadhi ya mamlaka zinazohusika kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda
pamoja na gharama ya nishati ya umeme kuwa ni kubwa hivyo hivyo watayachukua
mapendekezo hayo kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni ili serikali iweze
kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.
Pia alisema kuwa mapendekezo pamoja na
changamoto mbali mbali ambazo wamekutana nazo katika kiwanda hicho ikiwemo na
maeneo mengine ambayo tayari wameshayapitia watayawasilisha serikalini ili
yaweze kufanyiwa kazi ikiwemo na kutilia mkazo katika suala la usumbufu mkubwa
wanaoupata wawekezaji pindi wanapohitaji kuagiza matilio mbali mbali kutoka nje
ya nchi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zao.
Awali akitoa taarifa mbele ya
Kamati ya nishati na madini Mkurugenzi mtendajiwa wa kiwanda hicho cha
kuzalisha chuma, Haruni Lodhia amebainisha kwamba hapo awali walikuwa
wanakabilia na changamoto kubwa ya ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika
pamoja na miundombinu ya barabara,ambapo ameipongeza serikali ya awamu ya tano
kupitia Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa litafutia
ufumbuzi suala hilo na hatimaye kuanza utekelezaji wa kuzalisha bidhaa mbali
mbali, ikiwemo Nondo, mabomba ya maji na bodi za jasi.
Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda cha
Lodhia ambacho kinajishighulisha na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo
chuma, akiwaonyesha wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini jinsi ya
kiwanda hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuwaelezea changamoto mbali mbali
zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa serikali zifanyiwe kazi. (Picha na Victor Masangu).
Badhi ya wabunge wanaounda kamati ya
nishati na madini wakati wanaingia katika kiwanda cha kuzalishia chuma cha
Lodhia ikiwa ni moja ya ziara yao ya kikazi kwa ajili ya kuijionea shughuli
mbali mbali zinazofanywa na wawekezaji pamoja na kubaini changamoto zao, wa
kati kati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa. (Picha na Victor
Masangu).
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya
nishati na madini wakiwa na viongozi mbali mbali wa kiwanda hicho wakitembezwa
katika maeneo mbali mbali ili kuweza kujionea mwenendo mzima wa vyuma chakavu
vinavyoyayushwa na kutengenezwa Nondo mpya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbali mbali ikiwemo ile ya serikali. (Picha na Victor Masangu)
Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya
bunge ya nishati na Madini Vedastus Matayo akipokea maelekezo kutoka kwa mmoja
wa viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Lodhia kilichopo kata ya
Kisemvule wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipokwenda kwa ajili ya kujionea
shughuli mbali mbali za uzalishaji kiwandani hapo (Picha na Victor Masangu).
Mwonekano wa mtambo maalumu wa
kuzalishia nishati ya umeme wa gesi asilia ambao umefunngwa na shirika la
TPDC katika kiwanda hicho cha kuzalishia chuma pamoja na kutengenezea
mabomba ya maj wakati wa ziara hiyo ya kamati ya bunge ya nishati na
madin.(Picha na Victor Masangu)
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha
Lodhia Haruni Lodhia ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa kutengeneza
Nondo pamoja bidhaa zingine mbali mbali akizungumza mbele ya wajumbe
kamati ya bunge ya nishati na madini hawapo pichani ilipofanya
ziara ya kikazi ya kutembelea kiwanda hicho. (Picha na Victor Masangu)
No comments:
Post a Comment