Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi
wanawake wa serikali kuu na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catherine Katele
kulia akimkabidhi msaada wa magunia ya mahindi Katibu Tawala wa Wilaya ya
Rufiji Maria Katemana kwa ajili ya kuwapatia wananchi waliopata maafa ya
mafuriko kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
.......................................
VICTOR
MASANGU, RUFIJI
Baadhi ya wananchi Wilayani Rufiji Mkoa
wa Pwani wamekosa makazi ya kuishi kutokana na nyumba zao pamoja na
maduka kuzingirwa na maji ikiwemo wengine kukumbwa na changamoto ya
mazao yao mbali mbali zaidi ya hekta 4,000 kusombwa na maji kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha na kusababisha maafa ambayo yamepelekea wananchi kuishi
katika mazingira magumu hivyo kupelekea kuishi katika mazingira magumu.
Hayo yalibainishwa na wananchi
hao wakati wa ziara ambayo imefanywa na Wanawake wa chama cha wafanyakazi
wa serikali kuu na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani yenye lengo la
kutembelea baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na maafa ya mafuriko
kwa ajili ya kutoa msaada wa vyakula kwa walengwa.
Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati
tofauti akiwemo Shamte Ally na Said Salumu walisema walidai kwamba mvua
ambazo zinaendelea kunyesha kwa kipindi hiki zimewaletea hasara kubwa ya
mazao yao, mifugo, pamoja na makazi kuzingirwa na maji hivyo wameiomba serikali
ya awamu ya tano kuwasaidia msaada wa kupata chakula pamoja na
sehemu kwa ajili ya kuishi.
Aidha waliongeza kuwa kwa sasa kutokana
na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya bidhaa ya vyakula katika maeneo mengine
zimepanda bei hivyo wengine kutokana na kipato chao kuwa cha chini wanashindwa
kumudu gharama kwa ajili ya kununua vyakula hivyo wameomba wadau mbali mbali
kwa kushirikiana na serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho la tatu
katika kuwasaidia kuondokana na hali hiyo.
Kwa kweli ndugu waandishi kwanza
tunashukuru sana hawa wakinamama wa Tughe Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuja mpaka huku
katika maeneo ya Rufiji, kwani kwa sasa tupo katika hali ngumu sana kutokana na
mazao mbali mbali ya chakula ambayo ndio tulikuwa tunayategemea sisi pamoja na
watoto wetu yote wamesombwa na maji, lakini pia tunashukuru kupatiwa msaada huu
lakini bado tunahitaji zaidi ili tuweze kujikimu,” walisema wananchi hao.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya
ya Rufiji Maria Katemana alikiri kuwepo kwa maafa hayo na kubainishwa
kwamba hadi sasa zaidi ya hekta 4000 za mazao ya aina mbali mbali ikiwemo
mahindi mpunga, yamesombwa na maji ambapo pia kuna baadhi ya shule
nne za msingi zimefungwa kwa muda kutokana na kuwepo kwa hali hiyo
ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
“Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani
zangu kwa niaba ya serikali ya Wilaya ya Rufiji kwa msaada huu wa chakula cha
mahindi ambao umetolewa na Wanawake wa TUGHE Mkoa wa Pwani kwa lengo la
kuwasaidia baaadhi ya wananachi amabao wamekumbwa na mafuriko hayo ambayo kwa
kweli yamesabisha hekta zaidi ya 4000 za mazao kusombwa na maji na kuna
maeneo mengine ya shule bado maji yapo, hivyo tunaendelea kujitahidi kwa hali
na mali ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao, alisema Maria.
Kufuatia kutokea kwa maafa hayo
ya mafuriko Wanawake kutoka chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya
(TUGHE) Mkoa wa Pwani wameguswa na tukio hilo na kuamua kwenda kutoa
msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo mahindi kwa wananchi ambao wamekumbwa na
maafa ya mafuriko hayo kwa lengo la kuwasaidia kuweza kupata chakula
ikiwemo kupata mbegu kwa ajili ya kupanda tena kutokana na mazao yao yaliyosombwa
na maji.
Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi
wanawake wa serikali kuu na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catherine Katele
alisema kwamba waliamua kwenda kutembelea baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na
mafuriko na kutoa msaada wa vyakula kama mahindi ambayo yatawasaidia
wananchi kuweza kupata chakula na mengine kuyatumia kwa ajili ya kupanda
mazao mengine ambayo yamekwenda na maji.
“Sisi kama wanawake wa TUGHE Katika
Mkoa wa Pwani kwa kweli tumeguswa sana na jambo hili la wenzetu wa Rufiji
kupata maafa ya mafurikio, hivyo tukaona ni vyema tufunge safari ya kuja mpaka
huku na kweli tumejionea jinsi ya nyumba mbali mbali ambazo zimezingirwa na
maji na mazao ambayo yamesombwa na maji kwa hiyo kwa hiki kidogo tulichokitoa
cha msaada wa mahindi kitaweza kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine na pia
tutazidi kuendelea kutoa misaada mbali mbali kwa watu wenye mahitaji, “alisema
Katele.
Wilaya ya Rufiji iliyopo Mkoa wa Pwani
ambayo ina jumla ya kata zipatazo 13 imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya maafa
ya mafuriko hasa katika kipindi cha mvua zinaponyesha kutokana na baaadhi ya
maeneo kuwepo pembezoni mwa mto Rufiji hivyo kupelekea baadhi ya mazao kusombwa
na maji na nyumba nyingine kuzingirwa na maji na kusababisha wananchi kuishi
katika mazingira magumu.
Baadhi ya wanawake wa Chama cha Tughe
Mkoa wa Pwani wakiwa wanatoa msaada wa mahindi kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya
Rufiji akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wa serikali kwa ajili ya
kuwapatia wananchi ambao mazao yao yamesombwa na maji na wengine nyumba zao
kuzingirwa kutoka na mafuriko yaliyotokea. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Wanawake wa chama cha Tughe Mkoa wa
Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali
wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji mara baada ya halfa fupi ya
kukabidhi magunia ya mahindi lengo ikiwa ni kuwapatia wananchi ambao wamekumbwa
na maafa ya mafuriko na kusababisha mazao yao kusombwa na maji. (PICHA NA VICTOR
MASANGU).
Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria
Katemana akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa wanawake wa Tughe Mkoa wa
Pwani walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha na kutoa msaada wa
magunia ya mahindi pamoja na vyakula mbali mbali wa wananchi ambao wanamahitaji
kutokana na kupata mafuriko. (PICHA NA VICTOR MASANGU.)
Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi
wanawake wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catheline Katele akifafanua
jambo kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji hayupo pichani kuhusiana na ujio
wao wa kufanya ziara maalumu yenye lengo la kutoa msaada wa vyakula mbali mbali
ikiwemo magunia ya mahindi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko. (PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria
Katemana akiwa na wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa wanatembea kwa furaha
mara baada ya kumalika kwa sherehe ya kutoa msaada wa vyakula mbali mbali
ikiwemo magunia ya mahindi ambayo yametolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi
waliokumbwa na mafuriko (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya viongozi wa Tughe Mkoa wa
Pwani wakiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji wa kati kati wakipiga makofi
ikiwa ni ishara ya kufurahi mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa magunia ya
mahinda kwa waananchi waliokubwa na maafa ya mafuriko. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya wanawake wa Tughe Mkoa wa
Pwani wakiwa wanaimba nyimbo maalumu mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya halfa ya kukabidhi mahitaji mbali mbali
kwa wananchi ambao walipatwa na mafuriko na mazao yao kusombwa na maji na
wengine nyumba zao kuzingirwa na maji. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment