Mbunge
wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu pamoja na wazazi na walezi mara baada ya kukabidhi vitu hivyo vya magurudumu katika ofisi yake mjini Bagamoyo leo Tarehe 21 Machi 2020.
..............................................
Mbunge
wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa amekabidhi viti mwendo kwa
watoto wenye ulemavu wa miguu katika jimbo lake.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi viti mwendo hivyo, Dkt. Kawambwa alisema kuwa, viti mwendo
hivyo ni msaada kutoka kwa mama Janeth Magufuli hivyo anakabidhi kwa walengwa
ili kutimiza wajibu wake kama alivyooagizwa na mama Janeth Magufuli.
Alisema
Viti mwendo hivyo vitawasaidia watoto hao kutembea sehemu mbali mbali kwa kuendesha
wenyewe au kuendeshwa na kuondoa usumbufu wa kuwabeba hata pale wanapokuwa na
safari za lazima kama vile Hospitali Nk.
Aidha,
amewataka wazazi na walezi kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kuwahudumia
watoto hao kwa muda mrefu zaidi jambo ambalo litampa moyo yule aliyetoa na
kufikiria kutoa msaada mwingine.
Katika
hatua nyingine Mbunge huyo wa Jimbo la Bagamoyo aliwashauri kina mama wenye
watoto walemavu kuunda kikundi na kukisajili ili waweze kupatiwa mikopo ya
serikali inayotolewa kwa vikundi.
Alisema
serikali haiwezi kusaidia wananchi mmoja mmoja hivyo ni vyema wakiwa kwenye
kikundi ili waweze kupata mikopo inayotolewa na Halmashauri ambayo haina riba
na kwamba itawasaidia kujiendeleza kulingana malengo watakayojiwekea.
Dkt.
Kawambwa alitoa rai hiyo baada ya kina mama wenye watoto walemavu kumuomba
awasaidie wapate mitaji kwaajili ya biashara ili kukabiliana na malezi ya
watoto hapo.
Kwa
upande wao wazazi na walezi wa watoto hao wamemshukuru Mbunge huyo kwa
kufikisha viti hivyo kama alivyokabidhiwa na mama Janeth Magufuli.
Aidha
wamesema shukrani zimfikie mama Janeth Magufuli mke wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuwa moyo wa huruma na kuweza kufikiria kuwa kuna watu
wenye uhitaji wa vitu hivyo.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu pamoja na wazazi na walezi mara baada ya kukabidhi vitu hivyo vya magurudumu katika ofisi yake mjini Bagamoyo leo Tarehe 21 Machi 2020.
Mbunge
wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akizungumza na wazazi na walezi kabla ya kukabidhi viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu ofisini kwake Bagamoyo mjini
leo Tarehe 21 Machi 2020.
Mbunge
wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akizungumza na wazazi na walezi kabla ya kukabidhi viti mwendo kwa watoto wenye ulemavu ofisini kwake Bagamoyo mjini
leo Tarehe 21 Machi 2020.
Mbunge
wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, akikabidhi mfuko wa wenye spana zinazotumika kufungulia viti mwendo hivyo ikiwa vitaharibika ofisini kwake Bagamoyo mjini
leo Tarehe 21 Machi 2020.
Muonekano
wa viti mwendo vilivyokabidhiwa kwa watoto wenye ulemavu na Mbunge wa Jimbo Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa leo Tarehe 21 Machi 2020.
Kutoka
kulia ni Katibu wa Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Margret Joseph , Diwani wa kata ya Magomeni,
Mwanaharusi Jarufu, na Diwani wa viti maalum tarafa ya Mwambao, Shumina
Rashidi, wakati wa kukabidhi viti mwendo katika ofisi ya Mbunge wa Bagamoyo
dkt. Shukuru Kawambwa.
No comments:
Post a Comment