Mwenyekiti wa kikundi cha Pwani
Generation mwanamke sahihi wa kushoto akimkabidhi msaada wa vyakula mbali
mbali Lilian Mbise ambaye ni Mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima na wale
wanaoishi katika mazingira magumu cha Sharom kilichopo katika eneo la Kwa
mathiasi kata ya Msangani Wilayabi Kibaha,katika halfa iliyofanyika katika
kituo hicho.(PICHA NA VICTOR MASANGU).
...............................................
NA
VICTOR MASANGU, KIBAHA
Watoto yatima na wale wanaoishi katika
mazingira magumu katika kituo cha Sharom kilichopo kata ya Msangani
Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwasaidia
kwa hali na mali kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili ikiwemo
ukosefu wa mahitaji ya chakulai,nguo, huduma za matibabu pamoja na ujenzi
wa jengo la nyumba kwa ajili ya kuweza kuishi.
Baadhi ya watoto hao akiwemo Sara
Yendemba Dickson Michael wakizungumza
wakati wa halfa ya kupokea msaada wa mahitaji mbali mbali ikiwemo chakula
kutoka kwa kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi, walisema kwamba baada
ya kuondokewa na wazazi wao wamekuwa wanaishi katika mazingira magumu na
wakati mwingine walikuwa wanakwenda kutafuta chakula majalalani hivyo
wanahitaji msaada wa hali na mali kutoka serikalini na wadau wengine wa
maendeleo ili waweze kujikimu kimasiha kama watoto wengine.
“Tunashukuru sana kwa msaada wa vyakula
mbali mbali ambavyo tumepatiwa na uongozi wa wanawake wa Pwani
Generation kwani msaad huu utaweza kutusaidia, kwakuwa sisi hapa ni watoto yatima na wengine tunaishi
katika mazingira magumu, lakini tu bado tunamuomba Rais wetu aweze kutusaidia
zaidi ujenzi wa nyumba ya kulala kwani idadi yetu ni kubwa kuliko vitanda
vilivyopo”walisema watoto hao kwa masikitiko makubwa.
Pia waliongeza kwamba kabla ya
kufikishwa katika kituo hicho walikuwa wanaishi mitaani kwa shida kubwa sana
kutokana na kukabiliwa na changamoto mbali mbali ya kukosa mavazi, chakula
sambamba na mambo mengine muhimu lakini kutokana na kituo hicho angalau
wameweza kupatiwa hata fursa ya kwenda shule kwaajili ya kupata elimu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi
cha Pwani Generation mwanamke sahihi, Betty Msimbe amesema kwamba wameamua kutoa
msaada huo wa mchele, mafuta, unga, sukari, pamoja na maharage katika kituo
hicho kutokana na kubaini kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zinawakabili
watoto hao ambao wanahitaji kusaidiwa mahitaji mbali mbali ili waweze kujikimu
kimaisha.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba katika
kikundi chao wamekuwa na utaratibu wa mara kwa mara kwenda kutoa misaada katika
vituo mbali mbali vya kulelea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira
magumu vilivyopo katika Mkoa wa Pwani lengo ni kuwapatia mahitaji muhimu
ambayo wanastahili pamoja kwenda kuwafariji.
“Sisi kama Pwani Generation mwanamke
sahihi, tumeweza kubaini kuwa kituo hiki cha Sharom ambacho kipo katika Wilaya
ya Kibaha bado kinakabiliwa na changamoto mbali mbali na ndio maana tukaamua kukusanya
fedha na kuamua kununua mahitaji mbali mbali ambayo wanastahili kupatiwa watoto
hao kwani kutoa ni moyo na wala sio utajiri hivyo ni moja ya kuunga mkoni
juhudi za serikali katika kuwasaidia watoto,”alisema Msimbe.
Naye mlezi wa Kituo hicho Lilian Mbise
ambaye pia na yeye ni yatima amesema kwamba kituo hicho ambacho
kilianzshiwa tangu mnamo mwaka 2016 kina watoto wapatao 18 ambao wanaishi
katika nyumba ya kupanga hivyo kunahitajika msaada zaidi kutoka
serikalini kwa lengo la kuweza kuzitatua changamoto hizo zinazowakabili kwani
mahitaji yao ni mengi.
Kikundi hicho cha Pwani Generation
mwanamke sahihi, kilitoa msaada wa vitu mbali mbali, ikiwemo unga wa sembe,
sukari, mafuta ya kula, mchele,maji pamoja na mahitaji mengine ya msingi kwa
ajili ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha
Sharoom ambavyo vimegharimua kiasi cha
zaidi ya shilingi milioni moja.
Baadhi ya wanawake wanaounda kikundi
cha Pwani Generationi mwanamke sahihi wakiwa katika picha ya pamoja na watoto
wanaoishi katika mazingira magumu na yatima mara baada ya sherehe za kukabidhi
vyakula mbali mbali pamoja na mahitaji mengine ya msingvi katika kituo cha Sharom
kilichopo kata ya Msangani Wilayani Kibaha.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Baadhi ya watoto yatima na wale amabo
wanaishi katika mazingira magumu katika kituo cha Sharom kilichopo kata ya
Msangani wakiimba wimbo maalumu wakati wa halfa ya kukabidhiwa msaada wa
vvyakula mbali mbali kutoka na kikundi cha Pwani Generation mwanamke sahihi kwa
lengo la kuwasaidia watoto hao waweze kupata mahitaji muhimu.(PICHA NA VICTOR
MASANGU)
No comments:
Post a Comment