Mkurugenzi
wa shirika la Ocode Joseph Jackson wa kati kati akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa
Manispaa ya ubungo Beatrice Dominic wa kushoto pamona na Afisa elimu wa manispaa
hiyo kulia wakiwa wameshikilia upete kwa ajili ya kuukata ikiwa ni ishara
ya uzinduzi wa darasa moja la wanafunzi wa elimu ya awali Kibwegere ambalo
limetolewa na shirika la Ocode kwa ajili ya kuboresha sekta ya
elimu. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
..................................................
NA VICTOR MASANGU, UBUNGO.
SEKTA ya
elimu hapa nchini licha ya serikali ya awamu ya tano kuweka sera ya kutoa
elimu bure lakini bado katika baadhi ya maeneo ya shule za msingi na Sekondari
zilizopo katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam zinakabiliwa na
changamoto mbali mbali ya upungufu wa matundu ya vyoo pamoja na uhaba na
uchakavu wa miundombinu ya madarasa hivyo kusababisha wanafunzi wengine
kusoma katika mlundikano mkubwa.
Katika
kuliona hilo Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization Community
Development (OCODE) limeamua kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk.
John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa msaada wa
madawati 39,ya wanafunzi, viti 13 vya kukalia walimu pamoja na kukabidhi rasmi
chumba cha darasa moja jipya kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali
katika shule ya msingi Kibwegere.
Akizungumzia
kuhusiana na msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jackson amesema
kwamba kwa sasa wana tekeleza mradi wa elimu ambao utakuwa wa kipindi cha
miaka mitano ambao umeanza kufanyika tangu 2019- 2023 kwa lengo la kuweza
kuwasaidia watoto wa shule za awali na msingi katika kuwawekea mazingira mazuri
katika suala zima la upatikanaji wa elimu iliyo bora kwa manufaa yao ya baadae.
Aidha
Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba katika mradi huo umeweza kugusa ujenzi wa
darasa hilo jipya la wanafunzi wa elimu ya awali ambalo mpaka kukamilika kwake
limegharimu kiasi cha shilingi milioni 26 na kwamba wana imani kuwa watoto hao
kwa sasa waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya kukaa kwa mlundikano watasoma
katika mazingira ambayo ni rafiki kwao
“Shirika
letu la Ocode kwa sasa linaendelendea kutekeleza program ya mradi wa elimu
ambao utakuwa unazigusa baadhi ya shule za msingi ambazo zipo katika maeneo
mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam, maana nia yetu ni kuwasaidia watoto hawa
kuanzia elimu ya awali na kwamba kwa sasa tutajikita zaidi kwa wanafunzi wa
darasa la kwanza na darasa la pili pamoja na wale wanafunzi wa ngazi ya awali
ili kuweza kuwajengea uwezo wa kupata elimu bora,”alisema Mkurugenzi huyo.
Pia
alibainisha kwamba katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha
miaka mitano watahakikisha kwamba wanashirikiana bega kwa bega na serikali ya
awamu ya tano pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili kuleta mabadiliko chanya
ya kimaendeleo kupitia elimu kuanzia ngazi za chini na kuendelea.
Kwa upande
wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibwegre akisoma risala kwa mgeni
rasmi katika halfa ya makabidhdiano ya madawati na uzinduzi wa
darasa hilo amebainisha kwamba kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira magumu
sana kutokna na ukosefu wa ofisi za walimu na vyumba vya madarasa ambapo wakati
mwingine inawalazimu walimu kufanyia kazi zao wakiwa wamekaa chini ya miti
hivyo msaada huo ambao umetolewa na Ocode utakuwa ni mkombozi kwa upande wao.
“Shule
yetu ya Kibwegere kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa
Shirika hili la Ocode kwani wameweza kutuona na kutusaidia katika mambo mbali
mbali ya kutujengea darasa moja, kutupa viti, pamoja na madawati ya
wanafunzi hii kwa upande wetu ni moja ya hatua, kwani hapo awali hali ilikuwa
ni ngumu kutokana na miundombinu yenyewe ya madarasa pamoja na ofisi za walimu,
hivyo napenda kushukuru sana,”alisema Kulemba.
Kwa upande
wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika halfa ya makabidhiano hayo amesema kwamba pamoja na juhudi
zinazofanywa na serikali lakini amekiri bado kunachanagmoto kubwa ya
miundombinu ya madarasa kwa shule za msingi na sekondari na anatambua walimu
wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana hivyo amelipongeza shirika la
Ocode kwa kuamua kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu
kuanzia ngazi ya awali.
SHULE ya
msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo nje kidogo ya Jiji la Dar es
Salaam kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1741 ambao wanakabiliwa na
changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa walimu, uhaba wa miundombinu ya
madarasa, ofisi za walimu, pamoja na matundu ya vyoo.
Baadhi ya
wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibwegere elimu ya awali wakiwa
wameketi katika madawati ambayo yametolewa kwa msaada wa shirika la Ocode
katika halfa ya makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo
manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam, (PICHA NA VICTOR MASANGU).
Mkurugenzi
wa Shirika la Ocode Joseph Jackson akizungumza na baadi ya walimu, wanafunzi wa
shule ya msingi Kibwegere hawapo pichani wakati wa halfa ya makabidhiano ya
uzinduzi wa darasa jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya
awali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kusoma katika mazingira ambayo ni
rafiki. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkurugenzi
Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi
ambao walihudhulia katika halfa fupi ya makabidhiano ya chumba cha darasa jipya
ambacho kimejengwa kwa ajili ya kusomea watoto wa elimu ya awali. (PICHA NA
VICTOR MASANGU).
Mkuu wa
Shule ya Msingi Kibwegere Charles Kulemba akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi
wakati wa halfa ya uzinduzi huo wa darasa jipya mablo limejengwa mahusus kwa
ajili ya watoto wadogo wanaossoma katika ngazi ya awali. (PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Mmoja wa
walimu ambao wanawafundisha wanafunzi wa elimu ya awali Bi. Eunice Matembo
akisoma Risala yake kwa mgeni rasmi amabye ni Mkurugenzi mteandaji wa
Manispaa ya Ubungo hayupo picha wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano ya
madawati, viti pamoja na uzinduzi rasmi wa darasa hilo la wanafunzi wa
awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkurugenzi
mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic wa katikati akijadiliana
jambo na mwalimu mkuu wa Shule hiyo ya Kibwegere pamoja na watumishi wengine wa
Ocode na serikali wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano wa misaada mbali mbali
ikiwemo meza pamoja na viti kwa ajili ya kukalia walimu. (PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Baadhi ya
wanafunzi wa shule ya Msingi Kibwegere wakiwa wanasikiliza hotuba ambayo
ilikuwa inatolewa na Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson hayupo
pichani wakati wa sherehe ya uzinduzi wa darasa jipya ambalo limejengwa
kwa ajili ajili ya kuwasaidia watoto wa elimu ya awali. (PICHA NA VICTOR
MASANGU).
Baadhi ya
watendaji wa Shirika la Ocode wakiwa wameketi kwa utulivu wakifuatilia hotuba
ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic hayupo pichani wakati wa
halfa hiyo ya uzinduzi wa darasa moja jipya lililojengwa kwa ajili ya wanafunzi
wa elimu ya awali. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
Pichani ni
kibao ambacho kinaonyesha shule ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya
Ubungo iliyopo Jijini Dar es Salaam.abpo shule hiyo imepatiwa msaada wa
madawati, 39 viti 13 vya walimu pamoja na kukabidhiwa darasa jipya kwa ajili ya
watoto wa elimu ya awali lililotolewa na shirika la Ocode na kughalimu kiasi
cha shilingi milioni 24 (PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment