Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo wa kwanza akiwa katika moja ya eneo la chanzo cha maji
ya mto wami na kupokea maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Dawasa kuhusiana
na mradi huo wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kutembelea miradi
mbali mbali ya maji. (PICHA NA VICTOR MASANGU).
.......................................
VICTOR
MASANGU, PWANI.
ZAIDI ya wakazi laki moja wanaoishi
katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani ambao walikuwa
na kilio kikubwa cha miaka mingi ya kukosa huduma ya maji safi na salama
hatimaye wanatarajia kuondokana na kero hiyo sugu ifikapo Juni mwaka
huu 2020, mara baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa kutoka
eneo la ruvu juu hadi maeneo mbali mbali ya Chalinze ambao umegharimu
kiasi cha zaidi ya bilioni 16.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa
Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo katika ziara yake ya kikazi iliyolenga kukagua na kujionea miradi mbali mbali ya
ujenzi wa maji katika Wilaya ya Kibaha pamoja na mradi wa wami ambao upo
katika Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo na kuagiza mamlaka husika kuhakikisha
wanakamilisha mradi huo kwa wakati sambamba na kufikisha huduma hiyo
katika makazi ya wananchi pamoja na maendeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda.
Aidha Ndikilo amezitaka taasisi zote
kuhakikisha zinaachana na vitendo vya kuwa ni moja ya vikwazo katika
kutoa vibali mbali mbali kwa wawekezaji wa wa viwanda wa ndani na nje na
badala yake washirikiane nao bega kwa bega katika kutekeleza azma ya serikali
ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
“Kwanza kabisa nimeamua kufanya ziara
hii kwa lengo la kuweza kujionea miradi mbali mbali ya maji katika maeneo ya
Mkoa wetu wa Pwani na kwa upande wangu nimeweza kujionea jinsi ya mwenendo
mzima, na kiukweli nishukuru sana mtendaji mkuu wa Dawasa pamoja sa safu yake
yote kwa kuweza kufanya kazi ambayo inatia moyo ya kutekeleza kwa vitendo
miradi ya usambazaji wa maji katika maeneo ya viwanda na kwa wananchi wenyewe
hii ni hatua kubwa sana katika Mkoa wetu,”alisema Ndikilo.
Pia alibainisha kwamba kukamilika kwa
miradi mbali mbali ya maji katika Mkoa wa Pwani kutaweza kuwavutia wawekezaji
wa viwanda kuwekeza katika miradi mbali mbali sambamba na kuweza kutoa fursa za
ajira kwa vijana hivyo amewaomba wamiliki wa viwanda hivyo kuhakikisha wanawapa
kipaumbele zaidi wazawa katika suala zima la upatikanaji wa ajira lengo ikiwani
ni kujiongezea kipato na kuondokana na wimbi la umasikini.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa Dawasa
Mhandisi Cyprian Luhemeja baada ya kutembelea baadhi ya miradi
ambayo ipo kwenye mpango wa kupatiwa maji ikiwemo viwandani amesema
kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba wanatekeleza kwa vitendo
azma ya kumuunga Mkono Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli, katika
kuwa na uchumi wa viwanda pamoja na kuwaondolea kero wananchi ambayo wamekuwa
wakiipata kwa kipindi kirefu kwa kuwasambazia huduma ya maji safi na
salama.
Mhandisi Luhemeja aliongeza kuwa katika
jitihada za kuboresha huduma ya maji katika maeneo mbali mbali Dawasa
iliingia mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa bomba kuu la kusafirisha maji
lenye umbali wa kilometa 59 kutoka katika mitambo ya ruvu juu hadi katika
kijiji cha Mboga kilichopo katika halmashauri ya Chalinze na utekelezaji wake
unaendelea vizuri.
“Ujazo huu wa mradi mkubwa wa kutoka
mlandizi hadi chalinze unatarajiwa pindi utakapomalizika utasafirisha kiasi cha
lita za ujazo milioni tisa na laki tatu kwa siku moja ambazo zitaweza
kuwahudumia wakazi wapatao laki moja na ishirini sambamba na maunganisho mapya
ya wateja zaidi ya elfu 18 ambao wataweza kunufaika na mradi huo.
Naye Mbunge wa Jimbo la Chailzinze
Ridhiwani Kikwete alisema kwamba wananchi wake kwa
kipindi cha miaka mingi wamekuwa na adha kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji
safi na salama hivyo kukamilika kwa mradi huo utaweza kuwa ni mkombozi mkubwa
katika maeneo mbali mbali ambayo yalikuwa yanakabiliwa na changamoto sugu
ya kutembea umbari mrefu kwenda kutafuta maji.
“Hapo awali wananchi wangu wa
chalinze walikuwa wana kero kubwa sana ya kipindi kirefu kutokana na ukosefu wa
huduma ya maji, maana walikuwa wanatembea umbari mrefu kwa ajili ya kwenda
kutafuta maji lakini napenda kumshukuru sana Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli
kwa kuweza kutoa kiasi hiki cha fedha ambacho kitasaidia kuleta neema kwa
wananchi hawa kwani kwa sasa wao wenyewe wanajionea jinsi ya utekelezaji wa
mradi huu na maswali yamepungua kabisa kila kona, alisema Ridhiwani Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani yupo katika ziara
yake ya kikazi ya siku mbili katika baadhi ya Wilaya kwa lengo la kugagua na
kujionea shughuli mbali mbali zinazotekelezwa katika miradi mbali mbali
ya maji ambayo imelengwa kuwafikia wananchi pamoja na maeneo ambayo yametengwa
kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na mambo mengine.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo akimpa maelekezo moja ya wahandisi ambao wanatekeleza mradi mkubwa wa
bomba la maji ambalo linatokea katika mitambo ya ruvu juu kuelekea katika
maeneo mbali mbali ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo (PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo kulia akifafanua jambo katika kiwanda cha kuchakata nyama kilichopo
katika kata ya Kongowe wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya
kutembelea miradi mbali mbali ya maji .(PICHA NA VICTOR MASANGYU)
Mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi
Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na
utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maji katika Mkoa wa Pwani ukiwemo ule wa
kutokea katika mtambo wa ruvu juu kuelekea chalinze ambao utagharimu kiasi cha
zaidi ya shilingi bilini 16.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani
Kikwete akitoa ufafanua kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuhisiana na mwenendo wa
ujenzi wa mradi wa maji ambao unatekelezwa na serikali kwa lengo la
kuowaondolea changamoto ya huduma ya maji wananchi.(PICHA NA VICTOR
MASANGU)
Mtendaji mkuu wa Dawasa Mhandisi
Cyprian Luhemeja kulia akimpatia maelekezo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Evarist Ndikilo wakati alipotembelea moja ya mradi wa maji ambao
utawanufainisha wawekezaji wa viwanda mbali mbali kikiwemo cha kuchakata
nyama katika eneo la Zegereni Wilayani Kibaha. (PICHA NA VICTOR ,MASANGU)
Pichani ni moja ya baadhi ya mafundi
wakiwa na mtambo ambao unatumika kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa
maji kutoka mtambo wa ruvu juu kuelekea katika maeneo mbali mbali ya Chalinze
Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani. (PICHA NA VICTOR MASANGU)
No comments:
Post a Comment