Na
Albert Kawogo.
Huku China ikiwa tayari imelipunguza janga la tatizo la corona kwa zaidi ya asilimia 90; ugonjwa huo tayari umeshaua watu zaidi ya 6000 nchini Italia.
Kwa
nchi ya Italia pekee yenye mnara mkubwa wa jedwali la vifo; Jumamosi iliyopita
walifariki watu 627 Jumapili watu 793 na leo hii Jumatatu hadi sasa wamefariki
601 idadi ya waliopoteza uhai Italia tangu corona iingie nchini humo siku 64
zilizopita ni watu 6077 huku kukiwa na wagonjwa zaidi ya 40000 vitandani.
Wastani
wa vifo 600 kwa siku ni idadi kubwa tunaona Waziri Mkuu wa taifa hilo Giuseppe
Conte akitoa maoni ya kukata tamaa kupitia ukurasa wake wa twitter.
Dunia
inapita katika wakati mgumu huku ikielezwa na kushuhudiwa kuwa huenda hili ni
janga kubwa la kibinadamu ambalo rekodi yake haitaweza kumithilika siku zijazo.
Hoja
kuu zinazoibuliwa na wanazuoni mbalimbali Duniani ni uwezo wa mataifa duniani
hasa Ulaya Asia na Marekani kukabili ghafla na dharura huduma za tiba kwa watu
wengi mahututi kwa pamoja.
Changamoto
hiyo imeelezwa kuwa ndio sababu kuu inayofanya wagonjwa wengi wa corona
kupoteza maisha kwenye nchi hizo tajiri Sana duniani.
Mataifa
haya yenye uchumi mkubwa Ulaya ambao ni sehemu ya wanachama wa Jumuiya ya Ulaya
EU ambayo ni Italia Ujerumani na Ufaransa zikiwa ni siku 70 sasa yameshindwa
kabisa kuibuka na mpango wa dharura wa kupambana na corona huku Taasisi ya Afya
ya Dunia WHO ikibainisha kuwa chanjo ya ugonjwa huo inaweza kuchukua mwaka
mmoja na miezi 5 yaani miezi 17 au zaidi.
Hali
hiyo inatuonyesha kwamba ni lazima uwepo mpango wa dharura wa kupambana kuenea
kwa ugonjwa huu Ulaya Asia Afrika na Marekani.
Taarifa
za Shirika la fedha la kidunia IMF zinaonya kuporomoka kwa uchumi duniani
kutakakotokana kushuka kwa kiwango cha uzalishaji viwandani na upungufu mkubwa
wa biashara ya kimataifa hasa ya mafuta gesi madini na mazao.
Hatua
hiyo pia itaathiri sana sekta ya usafiri wa majini na anga hasa mashirika
makubwa ya ndege hali itakayochangia kudhoofisha sekta ya utalii.
Pamoja
na kuwa Afrika haijafikwa na wagonjwa wengi lakini watabiri wa mambo
wanabainisha kuwa Afrika ndio itaathirika zaidi na ugonjwa wa corona kwakuwa
sehemu kubwa masoko yake ya nje katika biashara yanategemea nchi zilizoathiriwa
na ugonjwa huo huku baadhi ya nchi hizo bajeti zao zikiwa zinapata misaada ya fedha
na ruzuku za maendeleo kutoka kwa nchi waathirika.
No comments:
Post a Comment