Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto)
akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo.
Mhandisi
Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za
juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa maelekezo kewa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) maendeleo ya
daraja hilo wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.
Mhandisi
Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd inayojenga barabara za
juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati) muonekano wa ramani ya
daraja hilo na ujenzi unavyoendelea wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya
mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida
akishuhudia.
.............................
WAZIRI wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
leo amevamia mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara
jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea chini ya
Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya nchini Japan.
Akizungumza
katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi huo
ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa.
Prof. Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara
baada ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao
barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam.
Mradi huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku
ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya fedha hizo
shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la Ushirikiano wa
Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa shilingi Bilioni 8.3.
Muonekano
wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment