Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na kikosi cha Polisi
wanawake baada ya kukagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake
alipowasili mkoani Singida, kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha
na kuzungumza na askari na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi wa Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Singida, wakati alipofika katika Ofisi
ya Mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na
maofisa wa Jeshi hilo pamoja na kujua changamoto wanazokutananazo wakitekeleza
majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na askari na maofisa
wa Jeshi hilo na kuwataka wafanyekazi kwa kutenda haki na kusimamia misingi ya
sheria na taratibu, IGP Sirro yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi yenye
lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari na kujua changamoto
wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao. Picha na Jeshi la Polisi.
........................
Na Jeshi la Polisi Nchini
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, amemaliza ziara yake
katika mikoa ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida, huku akiacha morali
kwa watendaji wa Jeshi hilo hatua ambayo italiwezesha ieshi hilo kufanyakazi
zake kwa weledi katika kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu.
IGP Sirro, amefanya ziara hiyo ikiwa ni mkakati wake aliojiwekea tangu
alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi hilo kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza
na askari na maofisa ili kujua namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za
Polisi.
Katika mazungumzo yake IGP Sirro, amewataka askari na maofisa kutimiza
wajibu wao kwa kutenda haki na bila uwoga wala kumuonea mtu muhali jambo ambalo
litarahisisha upatikanaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii.
Hata hivyo, katika mabaraza ya kuzungumza na askari na maofisa baadhi ya
hoja kadhaa ziliibuliwa kwa baadhi ya askari waliopata nafasi ya kutoa mawazo yao,
ambapo IGP Sirro aliahidi kuzishughulikia mapema ili kuzidisha morari katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha, katika ziara yake IGP Sirro, alipata fursa ya kukutanana Wajumbe
wa Kamati za Ulinzi na Usalama ya mkoa huku masuala kadhaa ya kiusalama na
mbinu na mikakati ikijadiliwa katika kamati hizo na kuahidi kutoa ushirikiano
utakaowezesha kukabiliana na matishio mbalimbali ya kiuhalifu.
No comments:
Post a Comment