Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid
Mwanga, akijiandaa kuingia uwanjani hii leo Julai 15, 2017 kuchezesha mechi
kati ya Madiwani wa Wialya ya Bagamoyo na wakuu wa idara ikiwa ni uzinduzi wa
kombe la Mazingira litakalojumuisha timu
28 ikiwa ni 26 kutoka kata zote za Wilaya ya Bagamoyo na 2 ni makundi maalum, pembeni
yake ni washika vibendera ambao kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Bagamoyo,
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP- Adam Maro, kushoto ni Mkuu wa Gereza la
Kigongoni, Mrakibu wa Magereza, SP-Muyengi Bulilo, wakipena maelekezo kabla ya
kuanza kwa mechi ufunguzi katika Uwanja wa Mwanakalenge mjini Bagamoyo.
Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga,wa pili kulia, ambae ndiye aliyekuwa mwamuzi wa pambano la mechi kati ya Madiwani na Wakuu wa idara, akitoa maelekezo kwa washika vibendera wake, kulia ni Mkuu wa Polisi wilaya ya kipolisi Bagamoyo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP- Adam Maro, kushoto ni Mkuu wa Gereza la Kigongoni, Mrakibu wa Magereza, SP-Muyengi Bulilo, wakipena maelekezo kabla ya kuanza kwa mechi ufunguzi katika Uwanja wa Mwanakalenge mjini Bagamoyo.
Timu ya Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze na
Bagamoyo wakiwa tayari kuingia uwanjani
kupambana na wakuu wa idara za halmashauri za Chalinze na Bagamoyo katika mechi
ya ufunguzi uwnja wa Mwanankalenge hii leo tarehe 15 julai 2017.
Timu ya wakuu wa idara za Halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo wakiwa tayari kuingia uwanjani kupambana na madiwani wa Halmashauri za Chalinze na Bagamoyo katika mechi ya ufunguzi uwnja wa Mwanankalenge hii leo tarehe 15 julai 2017.
Mshika kibendera katika mchezo huo, Mkuu wa
Polisi wilaya ya kipolisi Bagamoyo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP- Adam Maro,akiendelea na majukumu yake katika uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo mjini.
Mshambuliaji wa timu ya wakuu wa idara akijaribu
kuwatoka madiwani katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa leo Tarehe 15 Julai 2017
katika uwanja wa Mwanakalenge ambapo katika mechi hiyo wakuu wa idara walitok
na ushindi wa mabao 2 -1 dhidi ya madiwani.
Mwamuzi wa Mechi ya ufunguzi kati ya Madiwani na
Wakuu wa idara, ambae ni mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanga (aliyeshika
mpira) akitoa timu uwanjani baada ya kumalizika ambapo Wakuu wa idara walitoka
na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Madiwani.
Watizamaji wakifuatilia mchuano katika uwanja wa
Mwanakalenge mjini Bagamoyo.
Katikati ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo, Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe, Happyness William Seneda wakifurahia
jambo na Mwenyeji wake kushoto, Mkuu wa
Wilya ya Bagamoyo, Majid Mwanga, katika uwanja wa Mwanakalenge Bagamoyo mjini, kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Bagamoyo, Fatuma Omari Latu.
No comments:
Post a Comment