Mkuu wa Mkoa wa pwani, Mhandisi Everist Ndikilo,
amekutana na kufanya mazungumzo ofisini na wawekezaji kutoka nchini China, Bw.
Chen TianHai na Bw. Zhu Yumin kutoka Kampuni ya AnhuiHuaxin Group.
katika mazungumzo yao wawekezaji hao wamelenga
kupata ardhi yenye ukubwa wa ekari 8 kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda kikubwa cha
kutengeneza Betri za Magari (Recycling of Acid Battery Lead, assembling of
Battery and producing new Acid Battery) ndani ya Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na bagamoyokwanza blog. Mkuu wa Mkoa
wa Pwani alisema Uwekezaji huo utakuwa wa dola za kimarekani Milioni 30 ambapo
ujenzi wa kiwanda peke yake utagharimu dola za
kimarekani Milioni 3.
Aidh, alisema Kiwanda
hicho kitakamilika katika kipindi cha miezi 5-6 kuanzia sasa na kitaanza
uzalishaji mapema Januari, 2018.
Mazungumzo hayo yamewahusisha
NDC ambao wana eneo la viwanda la TAMCO lenye ukubwa wa ekari 230 lililopo
Maili Moja mjini Kibaha, ambapo ni kitovu cha Mji wa Kibaha ambalo tayari
limeanza kuendelezwa kwa ujenzi wa viwanda mbalimbali.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kufuatia mazungumzo
hayo tayari Kiwanja chenye ukubwa wa 161.85m x 157.57m ambacho ni sawa na meta
za mraba 25,503 ( Ekari 5.20) kilichopo NDC TAMCO kwenye eneo la uwekezaji wa
viwanda Kibaha kimechaguliwa na wawekezaji kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa
kiwanda cha kutengeneza battery za magari.
Alisema kuwa, Mtaalam kutoka NDC pamoja na Mpima
Ardhi wa Halmashauri ya Mji Kibaha wakiwa na wawekezaji wanaweka kumbukumbu
sawa
za kiwanja hicho ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Kiwanda hicho
kitakuwa mkombozi kwa battery zote zinazoisha muda wake na kutupwa na pia
kitakuwa rafiki wa mazingira kwa kuwa battery za magari hazitatupwa tena na
kuharibu mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa pwani, Mhandisi Everist Ndikilo,wa pili kushoto akiwa na wawekezaji kutoka china ambao wanatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza Betri za Magari Mkoani Pwani.
No comments:
Post a Comment