Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo leo
tarehe 12.7.2017 ametembeea kiwanda cha Kiwanda cha Masasi Food Products Co Ltd
kilichopo Lulanzi Halmashauri ya Mji Kibaha.
Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa Ndikilo amejionea
Awamu ya Pili ya Upanuzi wa Kiwanda hicho ambacho kimepanuliwa ndani ya kipindi
cha mwaka mmoja uliopita.
Kiwanda hicho ambacho ni cha Maji safi na salama
ya kunywa kimepata mkopo kutoka TIB, na ambapo kwa sasa Kimekamilisha ufungaji
wa mitambo uliofanywa na wahandisi kutoka nchini China.
Aidha, Kiwanda hicho Kimeshafanya majaribio ya
awali ya kutengeneza maji na kuyafunga ndani ya chupa za ujazo mbalimbali na
kupasishwa kwamba kiko tayari kwa uzalishaji.
Kiwanda kitakuwa pia na uwezo wa kuzalisha maji
na chupa za kwenye "water dispenser".
Mkuu wa mkoa wa pwani Mhandisi Ndikilo alisema Kiwanda
hicho kimekamilika kwa asilimia 95, na
kwamba Kinatarajiwa kuanza uzalishaji ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akikagua mitambo inayotumika kuzalisha maji katika kiwanda cha Masasi Food Products Co Ltd
kilichopo Lulanzi Halmashauri ya Mji Kibaha.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Everist Ndikilo akikagua mitambo inayotumika kuzalisha maji katika kiwanda cha Masasi Food Products Co Ltd
kilichopo Lulanzi Halmashauri ya Mji Kibaha.
No comments:
Post a Comment