Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru
Jumanne Kawambwa,wa pili kushoto akipanga makundi ya kufanya usafi wa mazingira jana jumamosi Tarehe 29 Julay 2017. katika eneo la Beach Bagamoyo, wa kwanza kulia ni mwanae Maliki Kawambwa na wapili kulia aliyeshika kiuno ni mwanae Mariamu Kawambwa
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa,wa pili kushoto na wa kwanza kushoto ni mwanae Mariam Kawambwa wakiwa katika zoezi la usafi wa mazingira maeneo ya Beach mjini Bagamoyo, usafi ulifanyika jana jumamosi Tarehe 29 Julai 2017.
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, katikati akizungumza na wananchi eneo la Beach Bagamoyo mara bada ya kumaliza kufanya usafi wa mazingira hapo jana jumamosi Tarehe 29 Julai 2017, mwenye miwani kulia ni Diwani wa kata ya Magomeni, Mwanaharusi Jarufu, na mwenye miwani kushoto ni Diwani wa viti maalu,Mwambao, Hafsa Kilingo.
.............................
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne
Kawambwa, ameshiriki usafi wa mazingira na mazoezi ya viungo yeye na familia
yake wakiwa wamejumuika na wananchi katika mji wa Bagamoyo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mazoezi
ya viungo pamoja na usafi wa mazingira, Kawambwa alisema ameamua kuifanya kuwa
siku rasmi kujumuika na wananchi wake katika kumuunga mkono Rais john Magufuli
kuhusu swala la usafi wa mazingira.
Alisema jamii inapaswa kujenga tabia ya kufanya
usafi wa mazingira ili kuepuka magonjwa yenye kuambukiza kama kipindupindu.
Alisema kufuatia umuhimu huo ndiomana hata yeye
ameweza kutoka na watoto wake Mariam na Maliki ili nao washiriki usafi wa
mazingira katika jamii na kwamba waone umuhimu wa kushirikiana na watu wa aina
zote katika mambo mbalimbali ya kijamii.
Katika zoezi hilo la usafi alipata fursa ya
kuzungumza na wavuvi na wauza samaki katika ufukwe wa Bahari ya hindi Bandari
ndogo ya Bagamoyo.
Awali wavuvi walimueleza mbunge Kawamba kuwa
wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa soko la kuuzia samaki
hali inayopelekea kukaa juani na kunyeshewa
Kawambwa aliwaeleza wavuvi hao kuwa hivi karibuni
soko la kuuzia samaki litakamilika ili kuwaondolea adha ya kuhangaika na sehemu
ya kuuzia samaki.
Katika Bonanza hilo la usafi vikundi vya Jogging kutoka Dar es Salaam vikiongozwa na Uhuru Jogging kutoka Radio Uhuru viliungana vikundi vya Jogiging vya Bagamoyo ili kutekeleza usafi kwa Pamoja ikiwa ni ishara ya kujenga ujirani mwema kati ya vijana wa Dar es Salaam na Bagamoyo, ambapo kwa Bagamoyo wenyeji wao walikuwa ni Bagamoyo Jogging.
vijana wa Joging wakiwa katika zoezi la usafi mjini Bagamoyo
Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa, katikati akiwa ameungana na wananchi wake katika kufanya mazoezi ya kukimbia kala usafi hapo jana jumamosi Tarehe 29 Julai 2017
vijana wa maigizo wakimunyesha Mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dkt. Shukuru Kawambwa, igizo linaloonyesha madhara yatokanayo na uchafu.
No comments:
Post a Comment