Na.Farida Saidy,Morogoro
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP) wilbrod mutafungwa, ametoa
wito kwa wanachi mkoani humo, kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi
ili taarifa zote zinazohusu viashiria vya uhalifu vifanyiwe kazi mara
moja.
Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na
waandishi wa habari amesema hali ya mkoa huo ni shwari na kwamba hakuna
matukio makubwa yanayotishia usalama wa raia na mali zao, na kuongeza kuwa bado
wanaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na matukio ya kiuhalifu na
wahalifu.
Mutafungwa amesema katika msimu huu
wa sikukuu za krismas na mwaka mpya polisi mkoa wa morogoro wamejipanga vizuri
kuhakikisha wananchi wanahudhuria katika nyumba za ibada na kushiriki ibada za
kusherehekea siku hizi kwa utulivu na amani.
Hata hivyo, kamanda mutafungwa
amesisitiza kuwa kutakuwa na ulinzi wakutosha katika nyumba za ibada, majengo
ya serikali, benki, masoko, kumbi za starehe, viwanja vya michezo pamoja na
kuimarisha doria katika barabara zote kuu pamoja na barabara za mitaani, kwamba
kutakua na doria za masafa marefu, pamoja na doria za miguu na doria
zinazoambatana na wanyama wakali (mbwa wa polisi).
Katika hatua nyingine jeshi la polisi
limetoa motisha kwa askari wake ambapo walishiriki kuokoa maisha ya baba na
motto ambalo limetokea siku chache zilizopita katika maporomoko ya nguzo
campsite.
Kwa upande wake diwani wa kihonda
khamisi kilongo, ambapo ndio wanapoishi baba huyo na mwanaye amelipongeza jeshi
la polisi kwa hatua iliyochukua na kusema ni hatua kubwa katika kuleta hamasa
kwa askari katika kufanya vizuri na ameomba hii iwe zoezi endelevu kimkoa na
ikiwezekana hata taifa zima.
Onesmo kahemere ni miongoni mwa
askari walioshiriki uokoaji ameelezea jinsi hali ilivyokua ambapo amesema kama
askari licha ya kuwa alikua akitimiza wajibu wake lakini pia aliguswa
kibinaadamu kufanya hivyo.